Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uthibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA),akifafanua jambo katika mkutano wa kujadili namna bora ya kukabiliana na tatizo la ajali za barabarani,Kulia kwa Mkurugenzi wa SUMATRA ni Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira Wizara ya Uchukuzi,Bi. Tumpe Mwaijande.Kulia kwa Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhe.Pereira Ame
Silima (aliyevaa suti nyeusi)ni Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe na kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhe. Dkt. Emmanuel J. Nchimbi(Mb).
 Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi,Said Mwema akichangia jambo katika Mkutano uliowakutanisha Waziri wa Uchukuzi,Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe(Mb) aliyevaa suti nyeusi,na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhe. Dkt. Emmanuel J. Nchimbi(Mb) aliyevaa suti ya kaki.Mkutano huo ulifanyika Wizara ya Uchukuzi na kuwakutanisha SUMATRA,Jeshi la Polisi,Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Chuo Cha Taifa cha Usafirishaji(NIT), Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) na viongozi mbali mbali wa Wizara ya Uchukuzi lengo likiwa kujadili namna ya kukabiliana na tatizo la ajali za barabarani Nchini.
Waziri wa Uchukuzi,Mhe Dkt. Harrison G.Mwakyembe(Mb),akisisitiza jambo kwenye mkutano wake na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.Kulia kwa Waziri Mwakyembe (aliyevaa suti ya kaki) ni Waziri huyo wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhe. Dkt. Emmanuel J.Nchimbi(Mb),kulia kwa Waziri Nchimbi ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Bw. Mbarak Abdulwakil  na kulia kwa Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ni Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi Said Mwema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...