Assalam Aleykum Sheikh!

Nimeokota passport ya bwana ALPHONCE NYALALI MAYALA jana kwenye parking iliyopo opposite na Wizara ya mambo ya nje na Mahakama kuu/ Kivukoni front.

Nimejaribu kupata picha hii, lakini kwa taabu maana hapa nilipo kwa sasa sina camera, na umeme umekatika sikuweza ku scan. ila nimeipiga picha kwa kutumia laptop, hope itafikisha ujumbe.

Nikutakie swaumu njema,

Wabillahi taufiq,

Daudi Danda
0767/0713 44 53 48

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Nakupongeza kwa utu wako bwana Daudi, natumai utampata Nyalali muda si mrefu. Huo ndio uTanzania.

    ReplyDelete
  2. Anapatikana Wiazara ya Fedha, Idara ya Fedha za Nje, Jirani na Wizara ya Mambo ya Nje.

    ReplyDelete
  3. Hongera kaka kwa kuwa muaminifu hope mwenye nayo at apatikana. Pass za wadogo zangu ziliibiwa crdb mbagala na watu wakauchuna tu hata baada ya kufungua akakuta Hamna kutu hasirudishe tu Jamani so sad.

    ReplyDelete
  4. Umefanya vizuri kuiokota na kuihifadhi hadi kufikia hapa kuitangazia kwa aliyepotelewa na Passport hiyo, tunakushukuru kwa hilo la kuwa muungwana na muaminifu.

    Lakini mbona umeziweka wazi details zake zote, at least ungetumia maarifa yeyote yale ya kuziziba pasina kuzitia dosari yeyote, kuliko kuzianika hivyo, au japo ungetangaza tu jina kamili la aliyepoteza Pass hiyo na kuweka contact zako ili awasiliane na wewe then umkabidhi mwenyewe, nadhani ingekuwa vizuri zaidi na salama to avoid frauds.

    ReplyDelete
  5. Hakuna cha frauds wala nini, kama binadamu anatembea katika njia zilizonyooka, hakuna jambo la kuficha hapo.Ila nyie mnaofoji foji makaratasi ya kwenda kujilipua Ulaya,ndiyo maana mko chonjo na uhalali wenu, maisha ya kuishi kimizengwe. Ningeshauri wa sanii wetu waje na filamu inayoitwa ( KUISHI KIMIZENGWE) Zebedayo msema kweli

    ReplyDelete
  6. Siku nyingine kaikabidhi polisi au idara ya uhamiaji.

    ReplyDelete
  7. ipeleke idara ya uhamiaji ndio njia sahihi!

    ReplyDelete
  8. HK.

    This is the best alieiokota could reach,
    Ameipresent kama alivyoikuta.
    Huo u James bond wa kuzibaziba wala hakuufikiria. Kumkosoa might be disturbing to him. Mwenye nayo pia must be the best outcome kuliko angeenda na mlolongo wa ukiritimba.

    ReplyDelete
  9. Afadhali ametoa tangazo kwenye mtandao kuliko kuipeleka polisi au uhamiaji rushwa ilivyojaa bongo mwenyewe labda zingemtoka kabla ajaipata.

    ReplyDelete
  10. Nadhani tabia hii ni njema sana na sifa ya pekee kwa watatnzania. Mungu atusaidie tuiendeleze.

    ReplyDelete
  11. huyu jamaa amefanya vizuri kuitangaza ila inategemea wakati mwingine watu wanaogopa kutangaza vitambulisho/passport vya watu wakiokota maana hujui vimepotea kwenye mazingira gani, unaweza kuja kuunganishwa na kitu kisichokuhusu kwa uungwana wako tu ukakuponza.

    pia kwenye passport kuna sehemu ya kujaza ndugu/rafiki watakaopewa taarifa wakati wa ajali au dharura nyingine nadhani hii sehemu ni muhimu kujaza maana angekuwa amejaza basi angepigiwa simu mmoja wa hao watu wake na kupatikina kirahisi ila wengi wetu tunadharau maana pengine huyu jamaa hatembelei hizi blog

    ReplyDelete
  12. jamani kuna mtu anatembea na passport kila mahali hajawahi hata kwenda kenya. akichukua mpesa kitambulisho passport sijui hajui thamnai yake hivi hana kitambulisho cha kata

    ReplyDelete
  13. Inaelekea hiyo passport haikuwa na visa, kama ilikuwepo basi ya msumbiji.

    Mzee wa vimodo
    KISAUKE MADALE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...