Ankal, 

Mtindo wa mabasi kuondoka pamoja kama msafara wa 'vigogo' kutoka vituo vya mabasi ya kwenda masafa ya mbali kama kituo cha mabasi ya mikoani Ubungo, Dar-es-Salaam ni mtindo wa hatari na waajabu kabisa.

Ni kama vile madereva wa mabasi ya kampuni mbalimbali wanaanza mashindano ya mwendo kasi wa mabasi makubwa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. yaahi hiyo donation inatakiwa kuwafanya nini madereva na wenye kampuni? yaani hakuna sheria bongo na hata kama zipo not enforced so it all about civilization in bongo! when will the land and its ppl become civilized?

    ReplyDelete
  2. Muda wa asubuhi barabara ya morogoro iko busy sana hasa upande wa kuelekea katikati ya mji. Ninavyoona mabasi hutoka kwa msururu na kwa haraka kwa maelekezo ya polisi usalama barabarani ili yaipishe barabara hiyo iendelee kutumika kwa wananchi waendao katikati ya mji. Wakiamua kuruhusu kila moja( basi) kutoka kwa wakati wake, barabara hiyo itafunga. Hapa tunaona askari polisi yupo anaelekeza mabasi hayo yapite, na amesimamisha magari yaendayo mjini kwa muda.

    ReplyDelete
  3. MDAU ULIYETOA HII MADA NA VIDEO KWA MAONI YANGU SIDHANI KAMA KUNA TATIZO KWA JINSI HAYO MABASI YANAVYOTOKA HAPO UBUNGO STENDI. KWA SABABU YANATOKA KWA UTARATIBU UNAOSIMAMIWA NA TRAFIKI. NA KWA TAARIFA NI KWAMBA YANAANZA KUACHANA BAADA YA KUFIKA KIMARA KWA SABABU KUNA AMBAYO YANASIMAMA KATIKA VITUO MBALIMBALI KABLA YA KUFIKA MBEZI AU KIBAMBA HUWEZI KUKUTA YAPO KATIKA MSAFARA KAMA WALIVYOTOKA UBUNGO. HATA HIVYO AJALI ZINAZOTOKEA SIO KAMA ZINASABABISHWA NA HUO MFUATANO HAPO UBUNGO STENDI BADALA YAKE ZINATOKEA HUKO NJIANI NA NJE YA MKOA WA DAR. NI MAONI YANGU TU HAYA ANKAL

    ReplyDelete
  4. Sijaona cha ajabu wala hatari hapo. Yanatoka kwa kuongozwa na askar wa usalama barabarani.

    Hapo kuna magari yanaenda more than 800km. Huo ndo mda mzuri wa kutoka.

    Mdau sikujua umetaka nn. au ndo unaonyesha ma-uwezo ya power point na uchuaji video?

    ReplyDelete
  5. Mwombeni Kingunge awachangieni!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...