Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa akifungua mkutano maalum Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha leo jijini Dar es salaam . Katika salamu zake kwa wafanyakazi amewaagiza kuweka mfumo mzuri wa ulipaji mishahara ili kuepuka malipo kwa watumishi hewa na kuongeza kuwa watakaoshiriki katika malipo hewa watachukuliwa hatua kali.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanyakazi wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah akimkaribisha Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa (hayupo pichani) ili afungue mkutano maalum Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha leo jijini Dar es salaam.
Wajumbe wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Wizara hiyo mara baada ya ufunguzi wa mkutano maalum wa Baraza la Wafanyakazi leo mjini Dar es salaam.Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO- Dar es salaam.





na joto lote amevaa sweta ndani. Kazi kweli...
ReplyDelete