Mkuu wa wilaya ya Korogwe Bw. Mrisho Gambo (wa kwanza kulia) Mkuu wa polisi wa wilaya hiyo OCD, Katibu Tawala wa wilaya hiyo pamoja na askari wakiandaa kuzichoma moto bangi walizozikuta katika nyumba kijiji hapo.
Mkuu wa wilaya Bw. Mrisho Gambo akimhoji bibi aliyekutwa katika kijiji hicho baada ya wana kaya wote kukimbia na kutelekeza nyumba zao katika kijiji hicho kwa kuogopa kukamatwa.
Mkuu wa wilaya akiwaongoza waandishi wa habari kuteremka katika mlima huo wa nyuma kabisa ni Bw. Mbonea Herman wa Tatv.
Mkuu wa wilaya akitoka katika kibanda cha nyasi ambacho alipofika usiku wa manane alijihifadhi humo kusubiri kuche ili ashirikiane na polisi kuwakamata wahalifu.
Bangi ikiteketezwa kwa moto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Huyu mkuu wa wilaya ni mfano mzuri kwa wenzake na watawala wengi. Anakubali kulala katika kibanda kama hicho huyu anastahili tuzo. hongera sana mkuu

    ReplyDelete
  2. now everybody is gonna get high, wish i was there...

    ReplyDelete
  3. Naitwa tajiri wa mawazo endelevu..tunataka viongozi wa vitendo kama huyu mkuu wa wilaya..hanautofauti na mwakiembe+magufuli.

    ReplyDelete
  4. kwa nini isiwe kama Columbia ruksa kujitafutia rizki ktk ufukara wa namna hiyo kijijini.

    ReplyDelete
  5. Kweli wamevuta moshi wa Bangi hawa waheshimiwa

    ReplyDelete
  6. Sasa huo moshi wake si ndio hapo kijiji kizima kitakuwa 'high' mkizingatia kuna na watoto wachanga, wazee na marika mengine tofauti pengine. Je, wote hao hawatoathirika na huo moshi wa 'Ganja' jamani. Unless kama lilitengwa eneo maalum lililo mbali na makazi/mazingira wanayoishi watu ndio zikachomewa huko, vinginevyo nadhani kwa siku hiyo haamki mtu hapo.

    ReplyDelete
  7. Hongera sana Kiongozi Mhe. Mrisho Gambo!

    Umefanya kazi nzuri sana, na iwe mfano kwa nchi nzima.

    Haya ndio matunda ya utendaji uliotukuka wa Viongozi vijana.

    Ma DC wazee hawana ujasiri wala uwezo wa kupanda milimani na kukabiliana na wakulima wa zao kumuenzi Hayati Bob Marley!

    ReplyDelete
  8. Enheee,

    Hiyo imekuwa ni free smoke!

    Direct MARLBORO!!!!

    Viongozi wakati mafusho ya ganja yanaungua hamkupata 'stimu' angalau kiduchu?

    ReplyDelete
  9. Enhhh

    Wakubwa baada ya msafara na kuitekekeza bangi kwa moto mliporudi Korogwe Mjini mlijikuta wooote mnacheza Reggae!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...