Ndugu zangu kuna mtu kaniomba nimsaidie kunyoosha hiki kiingereza kwenye hii barua, naomba muweke kwenye blog zetu tuwapate wataalamu kutusaidia na kutoa maoni yao.
Ila nimijiuliza "Jamani hawa ni watendaji wetu, hivi ni kwa nini wasitumie Lugha yetu ya kiswahili wakaeleweka vizuri? kwanza wanawaandikia watanzania wanaojua kiswahili kwa nini utumie kiingereza?
Vigezo vya kumpata huyu mtendaji vilizingatiwa?
Na hao walioko kwenye N.B Wameipata hii nakala na wakaafikiana nayo baada y kuisoma.
Aksanteni.
Hii hatari
ReplyDeleteInaonyesha "quality" ya elimu tuliyopata generations mbili au tatu zilizopita!!! Uozo mtupu.
ReplyDeleteHivi kulitokea maafa gani ya Ki-elimu Tanzania.
Tulikuwa a head above wenzetu Afrika Mashariki kwani tulikuwa na elimu ya kumuwezesha mtu kuzungumza na kuandika kiingereza fasaha kufikia darasa la nane. Kiswahili ni lugha mama yetu, ambayo nayo sasa tunababaisha babaisha tu. Lugha zote siku hizi zinatupiga chenga. Yaani hata wazungumzaji wa kiswahili cha pwani ambacho kilikuwa "standard" kwa lafudhi na matamshi siku hizi kimeoza.
Cha msingi hapa hakuna dawa ya haraka ndugu zangu. Huyu Bw. Mushi ataandika uwozo huo huo hata kwa lugha ya Kiswahili.
Itabidi tusubiri mpaka hizi generation zilizonyimwa "elimu" na wajanja wa Ujamaa zife kwanza ili tupate kizazi kipya. Hopefully watakuwa ni products za St. Mary's, Feza, na St Augustine's and such like institutions.
Peter Mushi hahahahahaaaaaaa! Nacheka kwa uchungu maana hii ni aibu kwa taifa. Duh! Na hao waliopatiwa nakala nao wakapitisha hoja bila marekebisho?!!!
ReplyDeletehayo ndio masuala ya kupeana kazi kindugu bila kujali qualification sasa mnaumbuka rekebisha mwenyewe
ReplyDeleteThis is a Disaster!Kwanini asiandike hiyo barua kwa Kiswahili?Aibu sana.Asirudie tena,tumemeza comments zetu!
ReplyDeleteHivi ilikuwa ni lazima atumie kizungu? Nembo ya barua pamoja na mhuri vimeandikwa kwa kiswahili kwanini ajifanya kuandika kizungu wakati kinamsubua. Ndio tatizo la kutojua kuwa hujui hilo. Maana angekuwa anajua kuwa kimombo hakijui asingetumia kiswahili na kujidhalilisha bila sababu.
ReplyDeleteHii ni aibu isiyokuwa na kipimo. Sio aibu tu kwa aliyeandika hii barua, bali ni aibu kwa Halmashauri ya Kinondoni na kwa Taifa zima.
ReplyDeleteTukubaliane kuwa mamlaka/elimu na lugha za kigeni ni vitu viwili tofauti, inategemea sana elimu yako uliipata kutumia lugha gani. Kutojua lugha ya kiingereza haitoi taswira halisi ya elimu yako. Hivyo kuhusu elimu tuachane nalo, tuangalie kuwa huyu jamaa uwezo wake wa kutafakari ukoje. Kwa wadhifa na mamlaka aliyo nayo anajijua kabisa kuwa hii lugha haijui.Hata kama kuna sababu zozote za msingi kuwa lazima barua iandikwe kwa kiingereza sio lazima aandike yeye, wapo wasasaidizi wake na hata wataalam wa lugha wa kulipa ili ujumbe uwafikie wahusika ipasavyo. Kuamua yeye aandike madudu huku akiwa anajua kuwa hii lugha inamtesa, inaonyesha jinsi alivyokuwa mjinga na mwenye kupenda kufanya maamuzi mepesi mepesi bila kutafakari. Hata hivyo kama hiyo lugha anaiona ni ya muhimu ofisini kwake asiwe mvivu ajisomee kwani kujifunza hakuna mwisho. Aibu tupu /shame on her/him
ReplyDeleteHahahaha..duh mbavu zangu!Yani barua nzima hamna hata sentensi moja iliyonyooka wala hata neno moja lililo sawa.Duh hii ni balaa.Haya ni matokeo ya kuanzishwa ualimu wa UPE na mambo kama haya yatanedelea kwa miaka kadhaa ijayo kwani ni miaka michache iliyopita tuliona walimu kusomea ualimu kwa miezi3 tena wale waliofeli kidato cha6 na kupelekwa kny shule za kata.Kazi ipo mbona,siasa bwana!
ReplyDeletejamani tumieni macrosoft word, inakurekebisha ukikosea spelling , hata sentence kama ina grammar mbovu inakushtua!
ReplyDeletethis is the badness of literally translation of swahili to english. what a mess! do we need to go back to school? let us appoint good educated guys in these places who can write well. he had a very good idea to inform the public knowing that dar es salaam is a commercial city whereby people from all over the world may converge here and let those who may not be able to understand swahili. but the opposite is true that the writer does not know english grammar. did his boss go thru this notice?
ReplyDeleteKabla hamjamkosoa kwanza mngetaka kujua alikua anataka kusema nini kiswahili na baadae mkakosoa.
ReplyDeleteNi lazima mjue kwamba huyo bwana kiingereza kwake ni second language, kosa kama hilo angelinya mdutch au mzungu yoyot mwengine kwa mfano mpolish mngeona kawaida. tujaribu kuwa positive kama anhaitaji msaada asaidiwe
Some one has to overhaul this letter, I mean we need to re-write the whole thing all over again.
ReplyDeleteImejikologa mno kupita kiasi, kwa hiyo haihitaji marekebisho bali inahitaji kuandikwa upya.
Na ni kawaida kwa form four wetu, wanakuwa hivyo siyo mbaya sana, anamsingi mzuri basi tu haja jiendeleza.
Kitendo hiki si cha kushangaza na wala sio mara ya kwanza ambapo lugha ya Kiingereza kinatumiwa ovyo na wala tena sio mara ya kwanza lugha ya Kiingereza kinapewa kipaumbele kwenye masuala ya kisheria au ya nayohusisha umma. Haieleweki kwani lugha kuu ambayo watanzania wengi wanaifahamu ni Kiswahili. Na kwa jambo la muhimu kabisa kama sensa ya watu na makazi, Kiswahili kinatakiwa kipewe kipaumbele kwa ajili ya kuwataarifu watu. Hii barua ingepaswa kuandikwa kwa Kiswahili na Kiingereza ili na wale ambao ni wakimbizi au wageni ambao hawaelewi Kiswahili wapewe fursa ya kujiunga na zoezi hili la mahesabu ya watu. Pia ni aibu kubwa kuona hali mbaya ya lugha ya Kiingereza inayotumika na hawa watu ambao wana vyeo vya aina fulani. Tunaweza kuwalaumu walio madarakani kwani hawajaweza kuhakikisha elimu bora kwa wananchi wote, lakini pia labda tujitazame sisi, wachache wetu waliopata fursa hii ya elimu. Je, tunafanyaje kuboresha Kiswahili chetu au Kiingereza chetu? Tunfanyaje kuwasaidia na wengine kupata elimu hii tulioweza kupata? Tunajishughulishaje na wanaharakti wa elimu kudai serikali na mashirika mengine husika kufikisha hizo fedha zinazotengwa kwa ajili ya wizara ya elimu? Wajibu ni wetu, vijana, tegemeo la taifa!
ReplyDelete"And such like institutions", anamalizia annony wa pili hapo juu akimcheka mwandishi wa tangazo hilo! Nyani amcheka mwenzie kundule!
ReplyDeleteNi mzawa MUSHI..... ndio watanzania wanavyofikiria siku hizi.Angekuwa ana asili ya kihindi, au kiarabu au kisomali mambo yangekuwa mengine. Tatizo liko moja tuchague watu kwa vigezo vyao sio nani anakujua au kabila ya mtu.Watu wengi educated, smart na wangeisadia nchi kufika mbali wamekimbia kwa sababu ya wachache kuendeleza mabaya yao katika uongozi, kwa kuwaweka watu wanaowapendelea wao. Kusudi wawalize. Na hope next time tukachugua mtu, tumuulize utafanyia nini wananchi, na kama ni mbunge awekwe kwenye mezani ya yote aliyoyafanya kusudi achaguliwe au hapana. Leo nchi zilizoendelea kama marekani ubaguzi upo, wachache wabaguzi wapo. Wengi hawana ndio maana hauonekani. Leo viongozi Tz wa kisiasa ni matajiri kuliko wafanyabiashara.The system is broken. Wananchi waamke na kuchagua watu bora, wazuri wakiwa wengi watabadilisha wachache. Tuache kufikiri mafanikio ni kujilimbikizia mali, tuangalie majirani zetu na wale wenye uwezo mdugu.Naomba samahani kama nitaonekana ni mbaguzi, kwa namna yoyote sio mbaguzi.Lengo langu watu wafakirie natural resourses zikiondoka ardhini hazirudi tena. Ni mali za watu, chini ya utanzania. watu wote wawe sawa under law. Mjerumani na mhindi ambao wana uraia watanzania, watoto wao wawe sawa na mtoto wa kichaga, au kabila yoyote nyingine. Obama baba yake ni kenya, leo ni rais wa marekani, nchi yenye wazungu wengi, na weusi ni less than asilimia 14%. Ulaya inaungana na africa tunagombania mipaka ya wakoloni. TZ ni nchi ya nne kwa africa to receive more aids from usa.
ReplyDeleteWadau wapendwa.
ReplyDeleteHii ni picha ndogo tu yakuonyesha hali ilivyo katika ofisi zetu za serikali hii. Inadhihirisha kuwa hata 'system' imeridhika na hali hii. hii ni aibu kwa aliyeandika, manispaa na serikali kwa ujumla.
tunaomba tamko kutoka kwa uongozi kinondoni kutueleza nini kinachoendelea?
Hata Nchi yake haijui. Republic Union of Tanzania ndio ipi hiyo?
ReplyDeleteJamani mimi naumwa kichwa....ngoja nikapate Aspirin...siweziii....karibia niukane uraia wa TZ...!!
ReplyDeletehuyu ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa, je anapatikanaje? na anatakiwa awe anajua kiingereza?ndio maswali tunatakiwa kujibu kabla ya kutoa mawazo yetu
ReplyDeletewengi wenu hapo juu ni small mind, yaani kanya boa watupu, ujuaji mwingiii lakini hakuna mlilolifanya kwenye jamii, hata hicho kiswahili chenu wengi mmekoroga koroga kuliko hata huyu jamaa mnayemkosoa. nimekaa na waingereza kibao na wao bado ni utata kuandika kiufasaha lugha yao,kama tunavyopata shida sisi kukiandika kiswahili.Je ?? cha ajabu hapa ni nini ??? kuna jamaa hapo juu kanikuna kweli ,baada ya kusema je ?? kama huyu mwandishi angelikuwa Mpolish au Mrusi aaa !! wala msingeropoka chochote, mngesema aaa !! huyo ni Mrusi english siyo lugha yake na yakaisha, sasa kwa mswahili mwenzenu imekuwa Fujo, hakusoma huyo, aibu tupu N.K acheni ujinga. zebedayo msema kweli
ReplyDeleteMMMMM?AIBU TUPU HII KWA JAMII JAMANI HUU UOZO MKUBWA,WEWE ULIYEANDIKA NENDA SHULE KASOME LUGHA MJINGA WA MWISHO WEWE UNATUAIBISHA.UNGEOMBA HATA VIJANA WA KIJIWENI WAKUSAIDIE KUANDIKA KIMOMBO KWANI WENGI NI WASOMI WAMEKOSA TU AJIRA.
ReplyDeleteDuh Nimesikitishwa sana na Mhishmiwa huyu. Ifike wakati tuangalie hili na mengine meeeengi yanayofanana na hili- Majina ya biashara zetu na uhalisia wake Meeengi ni ya kidhungu na Meengi dhaifu na saa nyingine hovyo yenye majina hayo ya kizungu - yenye maana tofauti na halihalisi ya shuhuli ama tunachotaka kusema! Je wanaotoa majina ya biashara zetu Bongo ni akina nani!km wakuta basi liendali mkoani limiandikwa jina Air..... Msae!! Hii Imikaaje!
ReplyDeleteJamani mimi ninaomba tusimlaumu Huyu Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa O'bay.
ReplyDeleteKwanza amejitahidi sana sana wapo watu wengi hawawezi kuandika hata hivyo alivyoandika huyu Mwenyekiti. na Alistahili kuandika hivyo maana hao wapiga kura wake ni Wazungu huenda au wasomi sasa ili kufikisha huo ujumbe vyema aliamua kutumua lugha hiyo.
Nampo pongezi sana na aendelee hivyo hivyo hadi kitaeleweka.
Kwa ufupi watu wengi mnakurupuka tu kutoa maoni. Ukisoma vizuri utangulizi, kabla ya barua hii kuwekwa, utaona kuwa hii barua haikwenda kama ilivyo, bali alipewa mdau kuirekebisha. Kwa hiyo iliyokwenda ilikuwa nzuri kama mdau ni mzuri kwa kimombo kumpita mwandishi mwenyewe. Lakini pia mdau ni MSHAMBA na si MTUNZA SIRI. Ni kwa nini aweke kwenye public kazi aliyopewa kumfanyia mtu? Shame up on you!!!
ReplyDeleteKaeleweka sioni cha ajabu!
ReplyDeleteWananchi mi nafikili tusimchambue Mushi kwa kuwa kasaini barua, kwa njia moja ama nyingine amechangia kiasi fulani kutopitia hiyo barua kabla haijasambazwa kwa wakaazi ambao kulingana na eneo wengi ni wageni. mimi nadhani secretary wa bw. Mushi ndio uozo kama walivyo ma secretary engi wa kitanzania. Miaka michache iliyopita nilipewa vyeti vya kuzaliwa watoto wangu toka kwa hao wanaojiita RITA majina yaliyokuwa kwenye vyeti namwachia mungu, na haya ni majina kama Wambura yaliandikwa Wamboro. Mungu ibariki TZ
ReplyDeleteNafikiri anatumia word ya zamani haina spell checker, au pengine hajua kutumia word. Msilaumu ni typo tu hizo.
ReplyDeletehahahahahahah...this made my day.
ReplyDeleteBora angeliandika kichaga Meku Ruwaaa.
ReplyDelete'Republic Union Of Tanzania, tafsiri=Jamhuri ya Muungano Tanzania'. huyu jamaa ametafsiri tu kiswahili to english, na ndio barua nzima ilivyo...kwa hiyo kama ujumbe umefika sioni tatizo, bali kwa huyo aliempa huo wadhifa alitumia vigezo gani, na je, huyu kiongozi hana wasaidizi???
ReplyDeletetujaribu kuangalia ufanisi wa kazi usiharibiwe na siasa zetu!
Hongera Mwenyekiti, ulichosema kimeeleweka ndiyo maana kimezusha mjadala mkubwa hapana tatizo kama mambo ya sensa yamekwenda vizuri na watu wamejiandikisha. Kosa la wasomi wengi serikali za mitaa hawazipendi kuzitumikia wanahisi hakuna ulaji, ila wape kule juu wawe wakitowa amri na mashangingi yako vivulini,nje koti ndani koti wanatoa hotuba hadi mate yanawakauka mdomoni;pia walinzi wako kila kona hawajui ya kwamba chini huku ndiyo taswira ya nchi yote. Komeni lawama zisizo na msingi, wazungu wa O'bay mbona wamemsoma vizuri? na ikiwa aliyepewa kuitengeneza ndiye aliyeitoa basi na yeye bwege tu, pia aibu kwake anaweza toa siri ya nyumba yake. watoa lawama wote na nyiye ombeni nafasi yake muone raha anayoipata ya kutoza ushuru hadi wa miguu ya kuku ili nyinyi mle kuku mzima. shame on you all,none sense.
ReplyDeleteIt seems this guy used Google translator from Swahili to English. There was a discussion on this blog last year about Tanzania education and the problem of English language in our education system. The government needs qualified English teachers to all elementary/primary schools. Form IV education is not enough for a person to be qualified to teach. In the West to be a teacher you must have a Bachelor of education, and that you have fulfilled all the requirements to be a teacher. It doesn't matter if you are going to teach pre-school or kindergarten. Tanzania education's system needs major overhaul!!!
ReplyDeleteKwanza kabisa, hiyo barua kiachapa katibu muhtasi wa Mzee Mushi, kwa msaada wa afisa wa chini wa hiyo ofisi.
ReplyDeletepili, barua hiyo ame saini Mzee Mushi bila ya kuipitia kukosoa.
tatu, barua imeandikwa kwa kiingereza (hichohicho cha lugha kongana) kwasababu ametaka ujumbe uwafikie wakazi wa huko Oysterbay!!! Maana wakazi wa huko wengi wao si wazawa, na Mzee Mushi aliona akitumia kiingereza, basi ujumbe utafika.
mekuu umefulia au ulionja kambege nini??
ReplyDeleteyerruuuuuuuuuuuuuuuuuuu.......!!!!!!
Alilazimika kuandika kingereza kwasababu maeneo anayo tawala yeye wanaishi Wazangu na watu wengi wasiojua Kiswahili.
ReplyDeleteMwenyekiti wa serikali za mitaa sio lazima awe anajua kingereza. Kwa vile yeye hajui alitakiwa kutambua kwamba hajui Kingereza na kuoma msaada wakati anaandika hiyo barua. Tatizo ni kwamba "hajui na hajui kwamba hajui" Vile vile yawezekana alijua kwamba hujui,ila akaona aibu kuomba msaada.