Kilimo ndiyo shughuli kuu ya uchumi Tanzania. NMB ikiwa benki yenye mtandao mpana zaidi Tanzania inatambua umuhimu wa kilimo kwa maendeleo ya Tanzania. Ili kuchochea maendeleo ya kilimo, NMB ilikuwa benki ya kwanza kuanzisha akaunti maalum kwa ajili ya wakulima iitwayo NMB Kilimo Account. Pia NMB imeanziasha huduma ya mikopo kwa ajili ya mazao mengi ya kilimo ikiwemo chai,kahawa,miwa,alizeti,korosho na mazao mengine.

 Ili kuelimisha umma juu ya huduma mbalimbali za kilimo NMB inashiriki kwenye maonyesho ya Nane Nane Morogoro, Dodoma, Arusha, Mbeya, Lindi na Songea, Tabora na Shinyanga. Akizungumza juu ya ushiriki wa NMB kwenye NaneNane Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NMB Imani Kajula amesema, “NMB inatambua umuhimu wa kilimo kwa maendeleo ya Tanzania ndiyo maana NMB imekuwa mstari wa mbele kubuni bidhaa na huduma maalum za sekta ya kilimo. Mbali na ushiriki NMB ni moja ya wadhamini wa maonyesho ya kitaifa yanayofanyika Dodoma”.

 Banda la Arusha

 Nane Nane Dodoma

Banda la NMB Morogoro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...