TAARIFA KWA UMMA
Tarehe 9 Agosti 2012 Gazeti la Rai Na.995 katika ukurasa wake wa kwanza lilichapisha taarifa yenye kichwa cha habari “Ufisadi Wizara ya Maji” na kuwa Viongozi Waandamizi wanatumia mali za Serikali na taaluma zao kwa maslahi binafsi. Gazeti hilo lilieleza kuwa walinzi wanashirikiana na wafanyakazi kula “dili” za nje, habari hizi hazina ukweli wowote na ni za kupotosha umma.
Maelezo yaliyoandikwa katika uk.2 na 3 chini ya kichwa cha habari hiyo, hakuna uhusiano wa Wizara ya Maji na ufisadi katika hifadhi ya eneo la Ngorongoro ambayo inamhusisha Mh. Pius Msekwa, Makamu Mwenyekiti wa CCM kama Mwenyekiti wa Bodi hiyo. Kwa maoni yetu Gazeti la Rai linawajibika kukiri kuwa kichwa cha Habari hiyo kilikosewa tena ukurasa wa mbele (front page) kama ilivyoandikwa habari hiyo. Tunaheshimu Uhuru wa vyombo vya Habari na tungependa kama kuna suala lolote linalohitaji ufafanuzi, Wizara ipo tayari muda wowote kutoa maelezo badala ya kukimbilia kuandika habari zinazojichanganya.
Imetolewa na
Katibu Mkuu
WIZARA YA MAJI
10/8/2012


Msijaribu kujisafisha Wizara ya maji nikweli ufisadi upo tena sana Swali moja tu mjibu vipi mnamlipisha mtu bili ya maji wakati maji hayatoki?mimi niko na kishoka anakaa hapo nje kinondoni amekushakuja na kunisawazishia bili mnazonibambikizia wacheni upumbavu wenu mnauwa nchi kwa ubinafsi wenu!
ReplyDeleteMh.Katibu inawezekana siyo wewe,lakini haya mambo yanafanyika huku chini,halafu hao hao ndiyo wanakuandalia hicho unachokanusha.Unaona mchangiaji wa kwanza alivyo na hasira??Tuwe wazalendo jamani,tumsaidie rais,haya mambo ya kutaka magazeti yaombe msamaha hayatusaidii lolote,na ndiyo yanayofanya tusiendelee.FAIFA LIMELIWA NA PANYA....PANYA HAWAKAMATANI..Kuna mtu katutungia shairi zuri humu kwenye blog.
ReplyDeleteDavid V
Hii taarifa kwa namna ilivyoandikwa mbona hovyo sana? Katibu mkuu wa wizara unashindwa kupangilia hoja zikakaa murua na kuvutia msomaji? Au uliiandika ukiwa na hasira/jazba?
ReplyDeleteDavid V pokea mapenzi makubwa. Ukweli ni uzalendo wetu pia utatu sadia. Tusonge mbele na umoja.
ReplyDelete