Mwenyekiti wa Bongo movie,Jacob Stevin 'JB' kushoto akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo (hawapo pichani) juu ya wizi mkubwa wa kazi za wasanii uliotokea hivi karibuni ambao ulibainiwa na Kampuni ya Steps Entatainment kwa kushirikiana na wasanii wenyewe na kudai kuwa tabia hii ikomeshwe kwa maharamia wa kazi za wasanii.katikati ni Rais wa Shilikisho la Filamu Tanzania 'TAFF' Simon Mwakifwamba na kulia ni Msanii Vicent Kigosi 'Ray'.
Msanii wa Filamu Nchini Mohamed Nice 'Mtunisi' kushoto akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati walipokuwa wanatoa tamko lao kwa waandishi wa habari kuwa wameungana kupambana na maharamia wa kazi zao.kulia ni Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama na Msanii Muhsin Hawadh 'Dk. Cheni'
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama katikati akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam baada ya wasambazaji kuungana na wasanii kwa ajili ya kutoa tamko la kupambana na maharamia wa kazi za sanaa.
Mwenyekiti wa Bongo movie,Jacob Stevin 'JB' pamoja na Rais wa Shilikisho la Filamu Tanzania 'TAFF' Simon Mwakifwamba wakionyesha baadhi ya kazi zao ambazo zimechakachuliwa na wajanja baada ya kuzikamata.Picha na Burudani Blog.

SHIRIKISHO la Filamu nchini(TAFF) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) pamoja Kampuni za usambazaji wa filamu na kazi za wasanii ‘zimeapa’ kupambana na maharamia wote wa kazi hizo ili kulinda maslahi ya wasanii.

Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo, umoja huo kwa pamoja ulisema umefika wakati tatizo la wizi wa kazi za wasanii lishughulikiwe kikamilifu ili kuzima mianya yote ambayo ni kero kwa muda mrefu.

Rais wa Shirikisho hilo Simon Mwakifwamba, mbali na mikakati hiyo pia aliiomba Serikali kutekeleza ahadi yake ya kuwasaidia wasanii kwa kupambana na maharamia hao aliodai kuwa wapo kila pembe ya nchi hii huku wakijiamini kwa kuendelea na kazi hiyo.

“Umefika wakati kwa Serikali kusikia kilio hiki cha wasanii na kuweka mbinu kali zitakazosaidia kuokoa maisha ya wasanii wanaoendelea kuwa masikini kila kukicha kutokana na uwepo wa watu wachache wanaoiba kazi zao”

“Tuna imani kuwa kama kazi za wasanii zitasimamiwa vizuri, tutaweza kuongeza pato la Taifa kwa kiwango kikubwa ikizingatiwa kuwa sanaa hii kwa sasa hapa nchini imeonyesha mafanikio isipokuwa kuna watu wachache ndiyo wananufaika nayo” alisema Mwakifwamba.

Naye Mwenyekiti wa Bongomuvi Jacobo Steven ‘JB’ alisema sanaa inaweza kuwa na nafasi ya tatu kwa kuchangia pato la Taifa ukiacha pato linalochangiwa na sekta za madini maliasili pamoja na utalii.

Alisema Serikali inapswa kuonyesha makali yake kwa kuwakamata wahusika wote wa wizi wa kazi hizo ili kuendeleza nguvu za wasanii wa hapa nchini walioamua kujitoa mughanga kufanya kazi zao.

Kwa upande wake Meneja usimamizi kutoka TRA Msafiri Ndimbo alisema Mamlaka hiyo imejipanga kudhibiti wizi wa kazi hizo kuanzia Januari Mwakani hasa baada ya Serikali kupitia Bunge lake kukubalina kuweka mikakati ya kupamba na suala hilo.

Ambapo wasanii na wasambazaji wa kazi zao wameungana pamoja kwa ajili ya kuhakikisha kazi zao zinakwebnda kwa haki ili wasanii wapate na wao wawe ni watu wa kusaidi wasanii kusambaza kazi zao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. hamuoni aibu nyinyi wenyewe kuwauzia watanzania michezo ya kuigiza alafu mnaiita film/movie? eti mnatoa film 10 kwa mwaka si wizi huo? JB acha hizo....
    kazi gani bwana mbona wengi hatuoni kazi yenu. marudio rudio tu.

    Mdau UK>

    ReplyDelete
  2. Na nyie acheni kukopi hadithi za ki-Nigeria na India

    Ignorant

    ReplyDelete
  3. Hawa jamaa kwa kweli chenga sana. Wenyewe kila siku wanaiba kazi za wenzao wa nje halafu wao "wakiibiwa" wanalalamika balaa! Mie hata kuangalia "movie" zao nishaacha maana hata hazina mvuto.

    ReplyDelete
  4. hayo maigizo mnayoyaita movie, mngeyaboresha ili yawe movie kweli. naungana na mdau hapo juu, kwenye movie mtu anapayuka utadhani ni ngonjera hilo lirekebisheni, na mambo ya kufanya ati kila movie ina kuwa na part one hadi 4 huo ni wizi mtupu, mbona hatuoni za kina rambo zikiwa na huo upuuzi wa part.. part.. acheni hizo. vinginevyo mtaendelea kulizwa kila siku manake na nyinyi mnaibia watu kisanii zaidi. ati kwa mwezi mmoja mtu anatoa movie 3 loh! mmeingilia fani za watu kwa pupa, jipangeni vizuri. au muende mkasomee hii fani ili mpanue upeo zaidi na muweze kujua mlikuwa manakosea wapi kuliko sasa hivi, haya maigizo mnayoita movie hayana mvuto. na wa kina dada wajifunze kuvaa kuendana na uhalisia wa kitu maana nguo ya ofisini mtu anavaa nguo ya kuendea club halafu vifupii vinabana vimewashika haswa, kweli mnaitaji darasa. ni hayo tuu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...