Kikosi kamili kilichowakilisha Tanzania kwenye michuano ya Olimpiki kikiwa na viongozi wao kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam leo jioni mara baada ya kuwasili.
Mwakilishi wa Mchezo wa Ngumi Selemani Kidunda. |
Wawakilishi wa Mchezo wa kuogelea Amal (mbele) Gadiale na Magdalena Moshi wakiwasili. |
Rais wa Kamati ya Olimpiki Filbert Bayi, akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Michezo nchini Leonard Tadeo ambae alifika kuwapokea uwanjani hapo. |
Katibu Mkuu wa Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT)Makore Mashaga akisalimiana na baadhi ya wawakilishi wa Tanzania kwenye michezo ya Olimpiki mara baada ya kuwasili nchini.


Wanalakiwa kwa shangwe kwa lipi hasa?
ReplyDeleteKwa shangwe na vigelegele wameleta medali ngapi?
ReplyDeleteWamelakiwa kwa shangwa kwa lipi jema au zuri wamefanya kule? mimi sikuona chochote cha kuvutia kutoka kwa hawa jamaa zetu.
ReplyDeleteMmmmh....sina cha kusema ngoja ninyamaze tu.
ReplyDeleteduu kumbe tanzania kuna hadi mkurugenzi wa michezo. sijui anaongoza nini wakati kila mchezo ni zero
ReplyDeletekwa shangwe???????mawefanya lipi la maana?????????
ReplyDeleteKitaifa hatuna cha kujivunia kutokana na ushiriki wao. Ila kwa wao binafsi na familia zao mambo mazuri, mwenye mabegi machache ni manne!!!
ReplyDeleteAFADHALI MMERUDI JAMANI. HONGERENI HAJAJILIPUA. TUNZENI HESHIMA YA NCHI. HATA KAMA HATUNA MEDALI HESHIMA YA TANZANIA PALE PALEEE! TANZANIA OYEEEE! WHO WANTS MEDALS!
ReplyDeleteDu nimeamini huyu bondia alikuwa shopping mibeg yote hiyo na amewrap up ili asiibiwe alivyoshop London!!
ReplyDeletetuache ubinafsi, sio wote walioshirika wamepata medali....hongereni. karibuni nyumbani. nyie ni mashujaa wetu. pamoja na maandalizi duni mmepambana mpaka mwisho
ReplyDeletewaogeleaji nilipenda ufanisi wao wakazane na mazoezi Brazil 2016 watafanikiwa...kila la kheri
ReplyDeleteWANAWAPOKEA KWA LIPI NZURI?MMETULETEA AIBU KUBWA NYIE,ANGALIENI KENYA UGANDA WALIVOFANYA MAMBO MAZURI.NYIE MMEKUJA KUANGALIA JIJI LA LONDON.
ReplyDeleteWamelakiwa kwa shangwe na vigelele kwa shopping walizofanya London, ndicho kilichowapeleka,simnaona hiyo misanduku ilivyo mingi na mikubwa?Kazi kwelikweli, hongereni kwa shopiing kubwa.
ReplyDeleteWelcome back our beloved TOURISTS!!
ReplyDeleteLabda Mashindano ya OLIMPIKI YA MAJUNGU NA UFISADI NA SIO YA MICHEZO ndio Tanzania itaibuka Kidedea!
ReplyDeleteOlympic in London:
ReplyDeleteDuuu hawa kweli wameenda Shopping!
Mibegi yote hiyo?
Haya ndio matokeo ya Ubabaishaji,Majungu,Rushwa na Upendeleo!
ReplyDeletePana mtoto mmoja ni Mkimbiaji mzuri sana kazi yake ni mwosha magari 'CAR WASHER' yupo pale Tancot House nyuma ya Luther House hapa Dar.
Huwezi amini Dogo aliwahi kukwamishwa ushiriki wa Mashindani ya Kimataifa akitakiwa atoe rushwa ya Tsh.500,000/= ili aingizwe katika safari!
Sasa je kwa mwosha magari anaweza kuwa na LAKI TANO ZA RUSHWA???
Nipo Krakow baada yakuwa pale Warsaw Poland na jamaa wengi hapa wananiuliza vipi Tanzania imepata Medali ngapi Olympiki naona Aibu jamani sina jibu. Wananiambia afrika Mashariki ni wazuri kwa ukimbiaji mie naguna hoi Tanzania nchi yangu. Haya Mola tusaidie tupate viongozi wajuu katika ngazi zakimataifa ila michezoni tupo hoi.
ReplyDeletewalikuwa wakinyimwa kula hawa bradford kila siku wanalalamika mlo mdogo hyo mogeleaji wa kike kamaliza wa 7 na wamwisho kwenye heat 2,afadhali wa kiume kwenye heat1 kamaliza wa tatu,ngumi na mengine sina lakusema vipi yule zakia amekimbia nin naona simuoni hapa maana ni mkimbiaji yeye isije kuwa kaonana na wakameruni?
ReplyDeletekwani kama mfuko wako ulikuwa safi usingefanya shopping????????? acheni wivu na majungu!
ReplyDeleteTatizo si shopping tatizo ni ............... wala sisemi malizini mkitaka
mi kama mwanachi mwenzenu, wachezaji fungeni mikanda ili mfanye mazoezi msisubiri mpaka mda wa mwisho. tunafanya makosa ya kufanya mazoezi tu pale mashindano yanapotokea na sio kila siku ndugu zetu nchi za jirani wanafanya mazoezi kila kukicha,
ReplyDeleteAssociation ya kila mchezo inabidi iamarishe wachezaji kuwa na mpango wa kufanya mazoezi ya kila siku sio tu pale mashindano yanapotokea.
Tobaaaaa?????? Hatutakaa tuendelee tanzania, hakuna fair kabisa, so sad
ReplyDeleteWanapokelewa kwa shangwe ya KUSHIRIKI.
ReplyDeleteSPORTSMEN SAY PARTICIPATING IS EQUALLY IMPORTANT.
Welcome back home guys, keep it up and stay fit.
Naona wote mnawalaumu ila hamtaki kusema ukweli sio sisi pekee ambao hatukupata medali kuna mataifa mengi hakupata kitu ila ukweli ni kwamba hatuna viongozi ambao wanaendesha shughuli za michezo kwa kujali kazi zao wao wapo kwa ajili ya manufaa yao uwaambie kufungua matamasha,na mikutano ya kila siku ya kulipana maalawansi tu.
ReplyDeleteMnakaa siku zote mnashindwa kuandaa wanamichezo na mapema kuanzia mashuleni mnakurupuka na kupeleka watu ambao hamkuwaandaa vya kutosha mnategemea nini kudra ya m/mungu.
Ni vyema uongozi wote wa michezo ukaundwa upya kwani hao wote waliopo wamekaa muda mrefu japo wengine waliwahi kuliletea sifa taifa huko nyuma,inabidi tubadilike sio kila kitu tunabahatisha tu