Kikosi kamili kilichowakilisha Tanzania kwenye michuano ya Olimpiki kikiwa na viongozi wao kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam leo jioni mara baada ya kuwasili.
Mwakilishi wa Mchezo wa Ngumi Selemani Kidunda.
Wawakilishi wa Mchezo wa kuogelea Amal (mbele) Gadiale na Magdalena Moshi wakiwasili.
Rais wa Kamati ya Olimpiki Filbert Bayi, akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Michezo nchini Leonard Tadeo ambae alifika kuwapokea uwanjani hapo.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT)Makore Mashaga akisalimiana na baadhi ya wawakilishi wa Tanzania kwenye michezo ya Olimpiki mara baada ya kuwasili nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Wanalakiwa kwa shangwe kwa lipi hasa?

    ReplyDelete
  2. Kwa shangwe na vigelegele wameleta medali ngapi?

    ReplyDelete
  3. Wamelakiwa kwa shangwa kwa lipi jema au zuri wamefanya kule? mimi sikuona chochote cha kuvutia kutoka kwa hawa jamaa zetu.

    ReplyDelete
  4. Mmmmh....sina cha kusema ngoja ninyamaze tu.

    ReplyDelete
  5. duu kumbe tanzania kuna hadi mkurugenzi wa michezo. sijui anaongoza nini wakati kila mchezo ni zero

    ReplyDelete
  6. kwa shangwe???????mawefanya lipi la maana?????????

    ReplyDelete
  7. Kitaifa hatuna cha kujivunia kutokana na ushiriki wao. Ila kwa wao binafsi na familia zao mambo mazuri, mwenye mabegi machache ni manne!!!

    ReplyDelete
  8. AFADHALI MMERUDI JAMANI. HONGERENI HAJAJILIPUA. TUNZENI HESHIMA YA NCHI. HATA KAMA HATUNA MEDALI HESHIMA YA TANZANIA PALE PALEEE! TANZANIA OYEEEE! WHO WANTS MEDALS!

    ReplyDelete
  9. Du nimeamini huyu bondia alikuwa shopping mibeg yote hiyo na amewrap up ili asiibiwe alivyoshop London!!

    ReplyDelete
  10. tuache ubinafsi, sio wote walioshirika wamepata medali....hongereni. karibuni nyumbani. nyie ni mashujaa wetu. pamoja na maandalizi duni mmepambana mpaka mwisho

    ReplyDelete
  11. waogeleaji nilipenda ufanisi wao wakazane na mazoezi Brazil 2016 watafanikiwa...kila la kheri

    ReplyDelete
  12. WANAWAPOKEA KWA LIPI NZURI?MMETULETEA AIBU KUBWA NYIE,ANGALIENI KENYA UGANDA WALIVOFANYA MAMBO MAZURI.NYIE MMEKUJA KUANGALIA JIJI LA LONDON.

    ReplyDelete
  13. Wamelakiwa kwa shangwe na vigelele kwa shopping walizofanya London, ndicho kilichowapeleka,simnaona hiyo misanduku ilivyo mingi na mikubwa?Kazi kwelikweli, hongereni kwa shopiing kubwa.

    ReplyDelete
  14. Welcome back our beloved TOURISTS!!

    ReplyDelete
  15. Labda Mashindano ya OLIMPIKI YA MAJUNGU NA UFISADI NA SIO YA MICHEZO ndio Tanzania itaibuka Kidedea!

    ReplyDelete
  16. Olympic in London:

    Duuu hawa kweli wameenda Shopping!

    Mibegi yote hiyo?

    ReplyDelete
  17. Haya ndio matokeo ya Ubabaishaji,Majungu,Rushwa na Upendeleo!

    Pana mtoto mmoja ni Mkimbiaji mzuri sana kazi yake ni mwosha magari 'CAR WASHER' yupo pale Tancot House nyuma ya Luther House hapa Dar.

    Huwezi amini Dogo aliwahi kukwamishwa ushiriki wa Mashindani ya Kimataifa akitakiwa atoe rushwa ya Tsh.500,000/= ili aingizwe katika safari!

    Sasa je kwa mwosha magari anaweza kuwa na LAKI TANO ZA RUSHWA???

    ReplyDelete
  18. Nipo Krakow baada yakuwa pale Warsaw Poland na jamaa wengi hapa wananiuliza vipi Tanzania imepata Medali ngapi Olympiki naona Aibu jamani sina jibu. Wananiambia afrika Mashariki ni wazuri kwa ukimbiaji mie naguna hoi Tanzania nchi yangu. Haya Mola tusaidie tupate viongozi wajuu katika ngazi zakimataifa ila michezoni tupo hoi.

    ReplyDelete
  19. walikuwa wakinyimwa kula hawa bradford kila siku wanalalamika mlo mdogo hyo mogeleaji wa kike kamaliza wa 7 na wamwisho kwenye heat 2,afadhali wa kiume kwenye heat1 kamaliza wa tatu,ngumi na mengine sina lakusema vipi yule zakia amekimbia nin naona simuoni hapa maana ni mkimbiaji yeye isije kuwa kaonana na wakameruni?

    ReplyDelete
  20. kwani kama mfuko wako ulikuwa safi usingefanya shopping????????? acheni wivu na majungu!
    Tatizo si shopping tatizo ni ............... wala sisemi malizini mkitaka

    ReplyDelete
  21. mi kama mwanachi mwenzenu, wachezaji fungeni mikanda ili mfanye mazoezi msisubiri mpaka mda wa mwisho. tunafanya makosa ya kufanya mazoezi tu pale mashindano yanapotokea na sio kila siku ndugu zetu nchi za jirani wanafanya mazoezi kila kukicha,
    Association ya kila mchezo inabidi iamarishe wachezaji kuwa na mpango wa kufanya mazoezi ya kila siku sio tu pale mashindano yanapotokea.

    ReplyDelete
  22. Tobaaaaa?????? Hatutakaa tuendelee tanzania, hakuna fair kabisa, so sad

    ReplyDelete
  23. Wanapokelewa kwa shangwe ya KUSHIRIKI.

    SPORTSMEN SAY PARTICIPATING IS EQUALLY IMPORTANT.

    Welcome back home guys, keep it up and stay fit.

    ReplyDelete
  24. Naona wote mnawalaumu ila hamtaki kusema ukweli sio sisi pekee ambao hatukupata medali kuna mataifa mengi hakupata kitu ila ukweli ni kwamba hatuna viongozi ambao wanaendesha shughuli za michezo kwa kujali kazi zao wao wapo kwa ajili ya manufaa yao uwaambie kufungua matamasha,na mikutano ya kila siku ya kulipana maalawansi tu.
    Mnakaa siku zote mnashindwa kuandaa wanamichezo na mapema kuanzia mashuleni mnakurupuka na kupeleka watu ambao hamkuwaandaa vya kutosha mnategemea nini kudra ya m/mungu.
    Ni vyema uongozi wote wa michezo ukaundwa upya kwani hao wote waliopo wamekaa muda mrefu japo wengine waliwahi kuliletea sifa taifa huko nyuma,inabidi tubadilike sio kila kitu tunabahatisha tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...