Baadhi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu mjini Mtwara,wakiwa katika hafla fupi ya kufuturu na kukabidhiwa misaada mbalimbali iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care & Share.
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mtwara Bw.Ponsiano Nyami akimkabidhi mfuko wenye unga wa kupikia ugali Bi.Chiku Mohamed aliepokea kwa niaba ya watoto yatima wa mkoa huo wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan Care & Share mjini humo inaendeshwa na Vodacom Foundation,wakati wa mfungo huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Shekh Mkuu wa Mkoa huo Nurdin Mangochi Mkuu wa Vodacom kanda ya kusini Bw.Mac Minja,Ofisa Mkuu wa Mauzo na usambazaji Bw.Hassan Saleh na Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule.
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mtwara Bw.Ponsiano Nyami,akimkabidhi mtoto yatima ndoo ya mafuta ya kula Bi.Halima Juma, aliepokea kwa niaba ya watoto yatima wa mkoa huo wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan Care & Share mjini humo inaendeshwa na Vodacom Foundation,wakati wa mfungo huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Shekh Mkuu wa Mkoa huo….Mkuu wa Vodacom kanda ya kusini Bw.Mac Minja,Ofisa Mkuu wa Mauzo na usambazaji Bw.Hassan Saleh na Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule.
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mtwara Bw Ponsiano Nyami,wapili toka kushoto pamoja na Shekh Mkuu wa Mkoa huo Bw.Nurdin Mangochi wakishuhudia Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji Bw.Hassan Saleh akimkabidhi ndoo ya mafuta ya kula mtoto yatima Bi.Mwajuma Khamis aliepokea kwa niaba ya watoto wenzake yatima wa mkoa huo wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan Care & Share mjini humo inaendeshwa na Vodacom Foundation,wakati wa mfungo huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule akimhudumia mtoto yatima Bi.Salha Haji uji mkoani Mtwara,aliefika kwenye hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan Care & Share inaendeshwa na Vodacom Foundation,wakati wa mfungo huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Baadhi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu mkoani Mtwara,wakifuturu wakati wa hafla fupi ya kufuturu na kukabidhiwa misaada mbalimbali iliyoandaliwa naVodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care & Share mjini humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera kwa kuwakumbuka watoto yatima na hii isiwe kwa mwezi huu tu, tunakuomba bw.michuzi uwe unaweka na anuani za vituo hivyo kwani kuna tulio mbali tunaguswa sana na jambo hilo lakini hatujui jinsi ya kufikisha misaada yetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...