Na Mwandishi Wetu

WANANCHI na wahanga wa bomoabomoa kwa wakazi wa nyumba za kota za eneo la Gerezani, Kariakoo, Dar es Salaam, wametahadharishwa kuacha kuchukua hatua yoyote kutokana na suala lao kuwa lipo mahakamani.

Wahanga hao wanasubiri kujua kama watafidiwa kitu chochote kutokana na bomoabomoa iliyowakumba hivi karibuni, na kupata fidia ya uharibifu na uvunjifu wa haki za wakazi hao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wakili Sengondo Mvungi, anayelisimamia suala hilo, alisema wakazi hao wanatakiwa kuwa watulivu kwa sasa kwani suala lao linashughulikiwa kisheria, huku akiwaahidi kulisimamia ipasavyo.

Mvungi, ambaye anatoka katika ofisi ya mawakili ya South Law Chambers, alisema suala lao litashughulikiwa bila kuwa na tatizo lolote likisimamiwa na yeye, na kuwasihi wanachi na wakazi wa eneo hilo kuwa na subira.

Alisema: "Suala la haki ya umiliki tajwa na fidia itokanayo na utwaaji wa eneo hilo na Serikali na fidia ya uharibifu na uvunjifu wa haki za binadamu za wakazi wa Gerezani ziko mahakamani kwa mujibu wa kesi namba 44 ya mwaka 2012."

Mvungi, alisema taarifa zilizotajwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usafiri wa Haraka (DART) kwa wahanga wakapokee fidia zao linakiuka amri ya Mahakama Kuu, iliyotajwa Juni 28, 2012, na kuwashauri kutotii agizo hilo.

Aidha, wakili huyo anayewasimamia wananchi wa Gerezani, amewataka kuhudhuria katika kikao cha pamoja na wakili wao (Mvungi), kitakachofanyika Agosti 11 mwaka huu (Jumamosi) katika ukumbi watakaoarifiwa na kamati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...