Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji mstaafu Joseph Warioba (kulia) na makamu wake Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani wakimsikiliza Mjumbe wa Tume hiyo, Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim (kushoto) leo katika mkutano wa Tume unaolenga kufanya tathmini ya kazi ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo unafanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es salaam.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Alhaji Said El-Maamry akiongea leo katika mkutano wa Tume unaoendelea unaolenga kufanya tathmini ya kazi ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo unafanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es salaam.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Ally Saleh akiongea leo katika mkutano wa Tume unaoendelea unaolenga kufanya tathmini ya kazi ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo unafanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es salaam.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Humphrey Polepole akiongea leo katika mkutano wa Tume unaoendelea unaolenga kufanya tathmini ya kazi ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo unafanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es salaam.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Awadh Ali Said akiongea leo katika mkutano wa Tume unaoendelea unaolenga kufanya tathmini ya kazi ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo unafanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es salaam.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Rishard Lyimo akiongea leo katika mkutano wa Tume unaoendelea unaolenga kufanya tathmini ya kazi ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo unafanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es salaam. (Picha na kwa hisani ya Tume)






Mm sikusoma lakini nimejaaliwa utajiri wa mawazo na mungu wangu..kwa hiyo mawazo yangu..ni kama hivi..1, mtoa rushwa na mpokeaji wote wanyongwe hii iwe kwa wote awe raisi au raiya awe kiongozi kifupi kila mtu hakuna rushwa.2, marufuku kwa kiongozi kua katika wizara ambayo hana ujuzi nayo..kwa mfano doctor anakua waziri wa michezo hapa wote tuseme nooooo..huyu anafaa kua katika wizara ya afiya.3,usarama wa taifa uwe mbele kulinda mari za taifa letu..4, raisi asiwe juu ya sheria na kuanza kupindisha pindisha katiba..5, jeshi liheshimu katiba..polisi wasajiliwe upya tena wasomi kuanzia kitato cha sita ili wawe na ufanisi na kazi yao..6, mtu akibaka wakina mama zetu dada zetu au wanafunzi wafungwe maisha na kila siku wachapwe fimbo mbili za nguvu..7,walimu.madoctor. wasifanye kazi katika mazingara magumu..8, marufuku kuluhusu ushoga..umaraya wa aina yoyote ile ili tuepukane na ukimwi na magonjwa mengineyo..9..njia za reli zijengwe kila mkoa..universty za kisasa kila mkoa..viwanja vya kisasa vya michezo...10, tuukatae katakata ukabira na udini..hayo ndio mawazo yangu na nnauhakika viongozi wetu watafika wakati watatuuliza mnataka nchi tuijenge vipi na tutawajibu kama za wenzetu..china..america...aksanteni wenu tajiri wa mawazo endelevu..amani kwa tz yetu.
ReplyDelete