Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya TAYODA, Jackson Kangoye, akikata mti kwa ajili ya kuandaa shamba katika kijiji cha Msagali, Mpwapwa mkoani Dodoma, juzi, taasisi hiyo inajihusisha na umahasishaji wa vijana kuingia kwenye kilimo badala ya kutegemea ajira serikalini.
Wananchi wa kijiji cha Msagali, Mpwapwa mkoani Dodoma, wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya TAYODA, Jackson Kangoye, hayipo pichani alipokuwa akizungumza nao juzi na kuwahamasisha kujiingiza kwenye kilimo.
Vijana wa kijiji cha Kibakwe, Mpwapwa mkoani Dodoma, wakianda shamba kwa ajili ya kuanza kulima. Vijana hao wamehamasishwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya TAYODA kujiingiza kwenye kilimo badala ya kusubiri kuajiriwa.

Na mwandishi wetu 

TAASISI ya Tanzania Youth Development Agenda (TAYODA), imesema mchakato wake wa kuanzisha benki ya vijana kwa lengo la kuwakomboa na kupata mikopo kupitia benki hiyo, unaendelea na upo kwenye hatua nzuri. 

Mkurugenzi Mtendaji wa TAYODA, Jackson Kangoye, alisema hayo juzi wakati akizungumza na baadhi ya vikundi vya vijana wilayani Mpwapwa, Dodoma ambao wamekuwa wakiwezeshwa na taasisi hiyo kufanya shughuli za kilimo na ufugaji. 

Alisema taaratibu za kuanzisha benki hiyo zimeanza na wameshafikia hatua mzuri na wanasubiri hatua za kitaalamu kuanza maandalizi ya kuifungua. Kangoye, ambaye pia ni mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Bara. 

alisema lengo la kuanzishwa benki hiyo ni kwa ajili ya kuwawezesha vijana kupata mikopo kupitia benki yao badala ya kutumia benki zingine. "Vijana wenzangu, taasisi yetu iko mbioni kuanzisha benki ya vijana, itakuwa mahususi kwetu na hivi sasa tumekutana na wataalamu wa masuala ya kibenki ambao watatushauri jinsi ya kuiendesha," alisema.

 Alisema baada ya kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa masuala ya kibenki, watakutana na baadhi ya vijana kuangali namna ya kuiendesha benki hiyo. Kwa upande wao baadhi ya vijana, walisema wamefurahishwa na uamuzi huo na wamewaomba viongozi wa taasisi hiyo kuhakikisha benki hiyo inafunguliwa kwa wakati. 

Said Husein, mkazi wa Kibakwe, alisema kuanzishwa kwa benki hiyo kutawakomboa vijana wengi ambao watakuwa wakipata mikopo kupitia benki hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Vijana hongera! Kwanza hakisheni mna pata hati za viwanja kabla kuwanza kulima.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...