Timu ya soka ya Veterans ya Golden Bush FC ya Shekilango jijini Dar es salaam  itakuwa  na mechi ya kirafiki  na timu ya Chuo cha ualimu Kigurunyembe siku ya Jumamosi mkoani Morogoro, kwa mujibu wa taarifa ya mmoja wa wachezaji  tegemeo wa Golden Bush FC bwana Onesmo Waziri “Ticotico” ni kwamba mechi itaanza saa kumi kamili katika viwanja vya chuo cha Ualimu Kigurumembe. 

Pamoja na kuondokewa na wachezaji wengi walioenda kwa mkopo kwe clubs mbalimbali kama vile Salum Sued (Mtibwa) Monja Liseki (Mtibwa) Herry Morris (Mbeya United) Amri Kiemba  (Simba), timu hiyo itategemea zaidi imahili wachezaji waliobaki kwenye timu kama vile Macocha Tembele, Ticotico, Hamis Msamba, Madaraka Seleman, Katina Shijja, Waziri Mahadhi, Abuu Mtiro, Yahaya Issa na golikipa namba moja bwana Zembwela. Baada ya game ya Morogoro mjini, Golden Bush itaingia kambini kujiandaa na safari ya kuelekea Kilombero kwa ajili ya kujinoa zaidi.

Imetolewa na Onesmo Waziri “Ticotico” mchezaji mwandamizi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...