Mdau Sunday Shomari akiwa na Mai waifu wake Elinita Mhando wakati wa kumeremeta kwao  leo katika kanisa la Mt. Emmaculata,Upanga jijini Dar es Salaam.
 Maharusi Sunday Shomari na Mai Waifu wake Elinita Mhando wakivishana pete ikiwa ni ishara ya kufunga pingu za maisha mpaka Mungu atakapowatenganisha.
 Padri akiongoza ibada ya Ndoa ya Mdau Sunday Shomari na Mai Waifu wake,Elinita Mhando mchana wa leo katika kanisa la Mt. Emmaculata,Upanga jijini Dar es Salaam.
 Maharusi na Wapambe wao wakifuatilia Ibada ya ndoa.
 Wapambee.
Maharusi na Nondozzzz zao.
 Maharusi katika picha ya pamoja.

AU  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. kweli siku hz ndoa ni makaratasi zaidi..enzi zetu ulikuwa huwezi kuonesha makaratasi ya ndoa (vyeti) hadharani..ni mwiko!!

    Babu Tiko- Greece

    ReplyDelete
  2. Beautiful...

    ReplyDelete
  3. Big up Sunday! Twakusubiri Washington Dc.

    ReplyDelete
  4. Homgereni sana maharusi na sunday usikose kuja houston kuja kupata BERBEQUE YA KUJIPONGEZA

    ReplyDelete
  5. yani mpaka msome kwenye madiko ndo mseme hisia zenu duu lakin nakutakiye kila la kheri na baraka tele sunday tunakusubiri d.c na maamaa tukufanyiye zinga la party mwamoyo ndo atakuwa kinara ha ha ha

    ReplyDelete
  6. umeshaoa sunday yani roho inaniuma si siri lakini nakutakia kila la kheri

    mdau idaho u.s.a

    ReplyDelete
  7. Hongera sana Sunday. Natamani ningekuwepo... ntakutafuta ukirudi USA.

    Babu Yake

    ReplyDelete
  8. Sunday ulikuwa bado tu? haya tulia na wako sasa.

    ReplyDelete
  9. Mdau wa idaho u.s.a Anonymous wa Sun Sep 30, 07:51:00 PM 2012

    Mara zote wanawake mikitakiwa mnakuwa mnanata sana na mapozi kibao, sasa wewe ulitaka akae Galacha ili uendelee kumdengulia?

    ......''umeshaoa sunday yani roho inaniuma si siri''

    Na wewe usipoteze muda bureee itazidi kukuuma la muhimu tafuta mwanaume wa kukuoa!

    ReplyDelete
  10. Anonymous wa Sun Sep 30, 07:51:00 PM 2012

    Wewe mdau idaho u.s.a

    ...Pole sana!,,,kitakuchoma kijiba cha roho!

    La muhimu usije ukajitutumua ukamvunjia ndoa Sunday Shomari inaoneka imekuuma sana na mara zote watu wa namna yako huweza hata kuhakikisha ndoa inavunjika ikiwezekana!

    ReplyDelete
  11. Mdau wa idaho u.s.a wewe Anonymous wa Sun Sep 30, 07:51:00 PM 2012

    Wakati Sunday mpo nae huko Marekani hukujitokeza kama ulikiuwa umapenda sasa ameoa inakuuma!

    Wewe ulitaka abaki Kapera ili uendelee kumdengulia?

    ReplyDelete
  12. mdau wa idaho u.s.a

    Anonymous wa Sun Sep 30, 07:51:00 PM 2012

    pole na uchungu bibie huko uliko Jimbo la Idaho kuna baridi saaana chemsha maji ya moto 'ujichue'!!!,

    Sunday huyooo na jiko lake ni siku chache utamwona huko Marekani anatesa kwa raha zake pika pakua!

    Tatizo kubwa dada zetu wa huko Majuu hasa Marekani wengi hamuoleki!

    ReplyDelete
  13. wewe Anonymous wa Sun Sep 30, 07:51:00 PM 2012

    mdau wa idaho u.s.a tatizo wewe 'gwinji' ama kwa jina lingine 'guberi' huoleki ndio maana Sunday amekuja kuchukua mke Tanzania badala ya wewe huko Idaho-Marekani !

    ReplyDelete
  14. mdau wa idaho u.s.a

    mtoa maoni wa nane (8) hapo juu, ITAKUUMA SAAANA,

    ...''utakufa nacho kijiba cha roho''

    ReplyDelete
  15. umeula wa chuya!!!

    sunday kwa sasa yupo kifuani mwa manamke mwenzio wa Tanzania anabembelezwa!

    wewe si uliringa?......mtoa maoni wa 6 hapo juu bibie mdau wa idaho u.s.a wewe ulitaka sunday aendelee kukaa na baridi ya marekani akiwa kapera ili uendelee kumtega?

    ReplyDelete
  16. Mwanamke wa Idaho USA wa sita hapo juu, kwa maringo na mikogo yako jamaa ameshindwa kukuona ingawa mko wote Marekani ndio maana amekuja kuoa Tanzania!

    Kwa nini usitafute Mzungu huko Idaho akuoe?

    Hizo si ndio zenu madadaz wa Kibongo? mnababaikia sana Wanaume wazungu matokeo yake mnakuwa hamuoleki, huku mkiona watu wanaoa nyumbani tena inawauma!

    ReplyDelete
  17. Kila la heri Kaka Mkubwa Sunday Shomari!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...