JUMAPILI ILIYOPITA MJOMBA WANGU ALIKUWA KWENYE DALADALA AKITOKEA UBUNGO KWENDA TEGETA.BASI LILIPOFIKA MWENGE ABIRIA WALIONGEZEKA NA WENGINE WAKAWA WAMESIMAMA,KATI YA WALIOSIMAMA ALIKUWAPO MZEE MMOJA ALIYEKUWA NA HAND BAG KAMA TUNAZOBEBEA LAPTOP HIVI, YULE MZEE ALIMUOMBA MJOMBA WANGU AMSAIDIE KUMSHIKIA BAG LAKE KWA KUWA YEYE ALIKOSA SITI, BILA YA KUSITA AKAAMUA MUMSAIDIA KALE KA BAG" BAADA YA VITUO VIWILI YULE JAMAA MWENYE KA BAG; ALITEREMKA BILA MJOMBA WANGU KUMUONA NA YEYE HAKUWA NA WASIWASI KWA KUWA ALIJUA MWENYE MZIGO AKITAKA KUSHUKA ATAUCHUKUA TU MZIGO WAKE.
KABLA GARI HAIJAFIKA KITUO CHA TATU ILISIMAMISHWA NA WATU WALIOJITAMBULISHA KWAMBA WAO NI ASKARI POLISI WAPELELEZI KWAMBA KUNA KITU WANAPELELEZA,WAKAWAAMURU ABIRIA WOTE WATEREMKE KWENYE GARI,WALIFANYA HIVYO MMOJA WA WALE POLISI, WALIMFUATA MJOMBA WANGU NA KUMUULIZA 'NA WEWE KWENYE BAG LAKO KUNA NINI? AKAWAJIBU BAGI SIYO LANGU KWA HIYO SIWEZI JUA NDANI KUNA NINI!! WAKAMUULIZA TENA, MWENYEWE YUKO WAPI TUONESHE" AKAANGALIA KATI YA WALE ABIRIA WENZAKE HAKUMUONA.
WAKASEMA FUNGUA TUONE KUNA NINI NDANI, WALIPOFUNGUA WAKAKUTA KUNA SILAHA AINA YA PISTO.ALIPOJARIBU KUJITETEA WAKAMWAMBIA TWENDE KITUONI UTAENDA KUJIELEZA HUKO. BASI LIKARUHUSIWA NA YEYE WAKAMPELEKA POLISI, WAKIWA NJIA WAKAMWAMBIA KAMA ANATAKA WAMWACHIE ATOE LAKI NANE 800,000/= VINGINEVYO WATAMUUNGANISHA KATIKA KESI YA WIZI WA KUTUMIA SILAHA,AKAWAAMBIA SINA HIZO PESA NA SIWEZI KUTOA MPAKA SASA BADO YUPO NDANI.HII INATUKUMBUSHA KWAMBA NI KWELI TUNAPENDA KUWASAIDIA WATU ILA TUWE MAKINI NA MISAADA TUNAYOITOA.
MZEE ALIKUWA NA NIA NJEMA KABISA YA KUTOA MSAADA ILA MSAADA UMEMGHARIMU MAISHA.
Mwisho napenda kuwatahadharisha watu wote tuwe makini na watu tusiowajua,
MTUMIE NA MWINGINE UJUMBE HUU
DAH! MWENYEZI MUNGU ATAMSAIDIA JAPO KUMZANIA MTU SIO VIZURI WATU WAKIKAMATWA NDIO STORY NYINGI KWA FAMILIA HUJITETEA, KAMA WANAOKAMATWA NA UNGA AIRPORT WAKISHIKWA HUSEMA JAMAA ALINIPA MZIGO SIKUJUA UNAKITUGANI, ILI WATU WASIONE ANA DILI ZA UNGA, ILA YA HUYU MJOMBA ATAKUWA KWELI WAMEMTEGESHEA MZIGO HUO NA VIPI POLISI KITUO CHA PILI AU TATU WAMEMSHIKA? MIE NA MASHAKA NA HAO POLISI PIA LAO MOJA NA MTU ALIYEMPA MZIGO MJOMBA! KAMA KASINGIZIWA MUNGU ATAMSAIDIA TU VUTENI SUBRA NA TUNASHUKURU NA USHAURI. M
ReplyDeleteKama nimeelewa vizuri inaonyesha huu mpango umepangwa na askari polisi. Kama hii ni kweli basi hapa tunaweza kujionea jinsi jeshi ili la polisi linapoelekea. Tunaelekea pabaya,kuna siku watu watawachenjia polisi wote..mimi yangu macho.Huu ni uonevu mkumbwa na hawa polisi hawana roho ya kibinadamu,ni wabaya kupita majambazi. Hapa walikuwa wanapora mtu pesa na hawaumii kuweka mtu ndani akaacha familia yake bila kosa na kumpa kosa la kufungwa miaka 30 kirahisi rahisi kwa ajili ya kupora laki 8
ReplyDeleteTATIZO hapo sio wema wa Mjomba, hasaa ni hao wanaojiita Police! naona ni ama wameweka njama kisa wapate hizo laki 8. mungu awamulike
ReplyDeleteHii moja kwa moja ni SACCOS ya Wana wa Makunjas!
ReplyDeleteHuo ni mpango kazi wa Polisi hakuna jingine isipokuwa wajiulize kweli njaa inapona kwa namna hiyo?
Mbona kesi ndogo waambie wampime mikono yake {finger print}kama siyo yake wa muachie hivyo waendelee kumtafuta mwenye mzigo!
ReplyDeleteUkisikia,
ReplyDeleteUgumu wa maisha kipimo cha akili...
Ndio hapa sasa.
Jamaa wanaona ili kuongezea mshahara ili kumudu majukumu wameona watumie akili hii.
Sasa panga la Laki 8 kwa Polisi hapo ni mshahara wa miezi mingapi?
Hii sasa ni pale mmacheza Drafti na Afande halafu anafosi kuingia KINGI!!!
ReplyDeleteNyie mliochangia hapo juu ni rahisi kudanganywa. Maana uelewa wenu ni mdogo. Hamuoni kuwa hii ni STORY ya kutunga tu?? Kama huyu MJOMBA bado yupo ndani, story ya kukabidhiwa begi ni sawa inaweza kuwa imetolewa na waliokuwa ndani ya daladala; lakini je ile ya kudaiwa laki nane, kaambiwa na nani?? Tunajua mtu akiwa ndani huwa ananyanganywa simu, pia ukienda kumwona, maongezi yanafanyikia hadharani, huku polisi wakiwa wanashuhudia. Jamani jaribu KUFIKIRI kidogo siyo kudanganywa kama MAZUZU. Hili halihitaji digrii ya falsafa ili kugundua kuwa ni STORY ya KUTUNGA.
ReplyDeleteTatizo sio polisi ni serekali, hao walipwe mshahara wa kutosha hawatafanya hayo wala kuchukua rushwa za kibwege bwege, pia madakatari na waalimu mbona bongo itakua shwariiii
ReplyDeletesema ndiko tunakoelekea,good things comes with big price to pay sometimes
pole mdau,sema chukua ushauri wa hapo juu waambie wacheck fingerprints.
Sasa hao polisi kama wako makini si waangalie fingure prints jamani!!
ReplyDeletekama unahitaji ukweli ni kwamba huyo mjomba wako ndie mwenye dili ya hiyo bastola hakuna mtu mwengine aliempa amshikie.Lakini kwa vile ameshaingia mtegoni anajaribu kupapatua.Bastola ni kitu cha thamani kubwa kuliko hizo laki nane anawezaje mtu mmoja mwenye bastola kuchukua daladala kisha kumuachilia mtu mwengine amshikie kitu chenye thamani kubwa kama hicho.kama unayo bastola niuzie mimi nitakupa millioni mbili bila kupatana.
ReplyDeleteHizi hadidhi za kale kawatolee watu wa mwanarumango na sio jijini.
Hii mbona kesi rahisi, ndugu yangu mpaka umeweza kuiandika hii kesi hapa kwa michuzi nadhani una uelewa mpana na uwezo wa kufuatilia mambo. Hao askari ni watuhumiwa namba 1, walijuaje kama katika hilo basi kuna mtu kabeba silaha? iweje waende moja kwa moja kwa huyo mjomba wako na kumkamata? sasa wageuzie kibao hao askari fuatilia upate masaada wa mwanasheria uwageuzie kibao hao askari washtakiwe kwa utapeli na pia usumbufu kwa mjomba wako na mwishowe watimuliwe kazi kwa kuliaibisha jeshi la Polisi. Ndugu yangu kila mtu ana haki yake, hakuna askari aliye juu ya sheria.
ReplyDeleteBy Bush lawyer
Mdau wa Sat Sep 15, 10:51:00 AM 2012
ReplyDeleteHahahahaha,!
Kama kucheza Drafti na Polisi ndio matokeo yake hayo kuwa anafosi kuingia KINGI na mimi leo mwisho nakaa karibu na Barracks Kurasini tunakaa nao Maafande Maskani tukicheza bao , sasa nitawatoroka!
Ahhh mnahangaika nini kuwaza ?
ReplyDeleteHiki ndio Kilimo cha Kisasa!
Na hii ndio MAFAO YA UZEENI KWA POLISI!
ReplyDeleteIpo kazi kama shughuli ndio hii unaweza kuja mtu kubebeshwa maiti ya Albino halafu ukakamatwa!
ReplyDeleteOhoooo, huu sasa sio U-Polisi bali ni Ujambaziiii !
ReplyDeleteKama ni mabao ya kufosi ndio hapa sasa mtu anakwenda na mpira golini filimbi ya kuotea inapulizwa mtu ndio kwanza anaachia shuti kali anafunga BAO !
ReplyDeleteHeee
ReplyDeletePolisi ni nyie tena?
Mmekula rushwa weee,
Mmewabambikia watu kesi weeee, Mmefanya kazi nje ya kanuni na taratibu za kazi weee,
Mmediriki kuwatoa maisha raia wema weee,
Kweli tutapona kwa mtaji huu?
Na sasa tena kwa kufosi mmekuja na funga mwaka ya M-Pesa kama VODACOM!
Mwambie mjomba wake mnakwenda kusoma albadili. Kama kasingiziwa, basi polisi mmoja mmoja watapukutika, ila Kama yeye mjomba ndiyo mguu wa kuku ni wake, basi jitaarisheni na msiba!! Hahahahahahahah....... Chezeni na psychology tu hapo!
ReplyDeleteMi sioni kosa la police, yawezekana wamepewa taarifa na msamalia mwema anayemjua mtu aliye na silaha akipanda basi hilo, kwani hali kama hizi hotokea sana tu! Kuhusu uhalali wa umiliki wa silaha nadhani finger prints itasaidia kumwondoa hatiani ikiwa hakuishika kwa mikono yake walipokuwa wanafungua begi kuangalia kilichopo. Lakini kitu nachoshangaa ni kwa nn aachiwe kitu chenye thamani hivyo? Ukweli ni kwamba aliyebeba begi hilo mwanzo(kama story inavyosema) hawezi kumkabidhi mtu mzigo kama huo angesimama nao tu pia hata kama angekabidhi hawezi kuusahau kamwe!! Otherwise talk to ur uncle in details
ReplyDelete