Katibu msaidizi wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro (MECKI) Dixon Busagaga akifanya utambulisho wa wageni kutoka klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Kagera (hawapo pichani) kwa mkurugenzi wa kituo cha radio cha sauti ya Injili.kushoto ni Mkurugenzi wa radio sauti ya injili ,Philemoni Fihavango na katikati hapo ni Katibu wa MECKI ,Nakajumo James.
Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari Kagera John Rwekanika (aliyesimama) akitambulisha waandishi alioambatana nao.
Mkurugenzi wa radio sauti ya injili ,Philemoni Fihavango akitoa historia ya wapi ilipotoka Radio Sauti ya Injili.
Watangazaji wa kituo cha radio cha Sauti ya Injili ,Moshi wakitoa maelezo kwa wanahabari wa mkoa wa Kagera,Kulia ni Suzane Ngeiyamu ambaye pia ni afisa uhusiano wa kituo hicho na kushoto ni Zawadi Mchome ambaye pia ni progarmu meneja.Mbele yao ni vifaa vilivyotumika kunasia sauti miaka mingi iliyipita ambavyo kwa sasa vinajulikana kama tape ama digital recoder.
Katibu wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro ,Nakajumo James akisikiliza radio ya zamani iliyoko katika kituo hicho.
Zawadi Mchome akitoa maelekezo katika studio ya radio hiyo ,aliyekaa ni katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Kagera,Phinias Bashaya.
Waaandishi wa habari mkoa wa Kagera na Kilimanjaro wakiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi wa kituo cha radio Sauti ya Injili Philemon Fihavango.Picha na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. radio sautu ya quran au al qaeda mnainaje ikija karibuni, si mtasema hawa wapiga maboni halafu leo hii tunaambiwa serikali haina dini na wimbo wa taifa si wa dini, unadhani bado tumelala au tukoko wafu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...