Ankal, 
Ilikuwa ni swala la kutia moyo kuwaona kwa wiki nzima wapinzani mbalimbali wakijumuika pamoja kwa amani. Maelefu ya Democrats, Republicans, Waandishi wa habari, waandamanaji, Wanaharakati mbalimbali pamoja na wavuta bangi walikuwepo kushiriki kwa njia mbali mbali katika Kongamanao la Democratic National Convention 2012. Maelufu ya walinda usalama nao walikuwepo . 

Hawakuonyesha kupendelea upande wowote au kumzuia mtu yeyote (isipokuwa wavunja amani) kutoa dukuduke yake. Kazi yao kubwa ilikuwa nikulinda usalama na amani ya wote walioshiriki. Nadhani huu ni mfano mzuri wa kuigwa 

 John Mashaka 
At The US-Democratic National Convention 
mashaka.john@yahoo.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hawa wote jina lao ni moja: NI BINADAMU. Hizo label mnawapa ninyi tu. Sijui wavuta bangi, republicans etc etc. Na inapokuja nchi wote wanasema: God Bless America!! Sio hapa mtu akishakuwa chama fulani, anakishikilia kama dini na kuona wengine kuwa hawastahili kuongoza au hata kuishi!!

    Ustaarabu bado sana huku daraja la tatu!!

    ReplyDelete
  2. Asante Bw.Mashaka.Tatizo watawala wetu hawataki kubadilika kwenda na wakati,hawajiamini,n.k Mimi nina Imani tutafika huko siku moja.

    Mashaka:Mbona kwenye hotuba za Michelle na Barrack Obama(DNC kwa ujumla) Camera zinamulika sana Wamarekani weusi,kunani au naangalia vibaya??

    David V

    ReplyDelete
  3. picha ya pili toka chini namuona huyo mzee democatic party strategist..da raha ya uchaguzi imeanza

    ReplyDelete
  4. Mheshimiwa mashaka. Kwanza kabisa nitasema kwamba unatuchezea kili zetu. Kuingia kwenye hizo DNC ni ngumu sana. Boss wangu ambaye amechangia chama cha Democracy hapa MD amejaribu sana kutafuta tiketi bila kufanikiwa. Kwa maana hiyo wewe hadi kupata hiyo tiketi wewe ni fisadi au wenzio walioangusha uchumi wa dunia wa Wall-street ndio wamekufanyia ufisadi. Nasema hivyo kwa sababu gani, wengine wanakuja kwa mialiko tu. Kwa hiyo kwa sababu porojo zako za kutupa lecture ya democracy wakati wewe umesoma bure DUKE university na kodi za watanzania utakuwa unatia aibu sana. CCM hawana shida na chama chochote na wala CCM haitumii polisi. wengi wa polisi wanajiopendekeza kutafuta vyeo ndio maana wanafanya makosa hapa na pale . mwisho hauwezi kulinganisha democrasia ya marekani na zile changa za kiafrika. na kama unaona udhaifu kwenue uongozi wetu, basi njoo ushiriki kwenye mchakato. Kutokana na umahiri wako, bila shaka CHADEMA watakupokea kwa mikono miwili hata CCM tutakupa ukuu wa wilaya au katibu tarafa. JK akikuonea huruma atakufa afisa ushuru TRA au Benki kuu, ikishindikana atakupa msaidizi wake wa uchumi pale magogoni.

    ReplyDelete
  5. Mashaka, you are an elitist completely out of touch.

    ReplyDelete
  6. NAUNGANA NA MKONO NA MIGUU NA AKILI ZANGU ZOTE NA MDAU ALIYE TOA MADA HAPO JUU KUMUITA MASHAKA NI FISASI NA NI KWELI KUINGIA KATIKA MKUTANO HUU SI MCHEZO NA WALI WANGI WALL STREET NI MAFISADI USISIKIYE MLIO NYUMBANI HAMUYAJUA HAYA NDO MAANA MNAONA BIG DEAL MTU AKIFANYA KAZI UN,WORLD BANK,WALL STREET ETC MNAMUONA WA MAANA SANA KUMBE EITHER NI FISADI AU ANA DEAL NA MAFISADI ILI KIBARUA CHAKE KISIOTE MBAWA NDO ILIVYO DUNIA, EITHER YOU BEND OR SOMEBODY IS GOING TO BEND YOU, UINAME UOKOTE AU UINAMISHWE UKOKOTESHWE,HAKUNA MTU YEYOTE MBABE KATIKA DUNIA HII AU VERY SMART IT WILL COME A TIME YOU WILL HUMBLE OR BE HUMILIATED TO BE HUMBLE NDO INAVYO KWENDA DUNIA

    SO MASHAKA USITULETE ZAKO ZA KULETAAAAAA

    MDAU BROOKLY MTANZANIA HAI NA ALIYE MAKINI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...