Na Veronica Kazimoto - MAELEZO, Mtwara.
Serikali
imetenga jumla ya shilingi bilioni mbili kwa ajili ya kufikisha umeme katika vijiji
vya mikoa ya Lindi na Mtwara ikiwa ni
mpango wa kufikisha miundombinu ya umeme katika vijiji mbalimbali kwa asilimia
therethini nchi nzima ifikapo mwaka
2015.
Kaimu Meneja wa Shirika
la umeme TANESCO Mkoa wa Mtwara Mhandisi
Daniel Kiando amewaambia waandishi wa habari kuwa fedha hizo zimetengwa kwa ajili
ya miradi therathini na moja (31) ambapo
vijiji vilivyopo katika wilaya za Masasi, Newala na Tandahimba vitanufaika.
"Mpaka sasa
tayari mradi umekamilika kwa asilimia mia moja katika kijiji cha Mbambakofi kilichopo
wilaya ya Tandahimba na wateja
wanaendelea kujaza fomu kwa ajili ya kuwekewa umeme katika nyumba zao,"
amesema Kiando.
Kiando
amefafanua kuwa nyumba zitakazowekewa umeme ni zile ambazo zimeezekwa kwa bati
hivyo ametoa wito kwa wananchi kuezeka nyumba zao ili waweze kunufaika na mradi
huo pamoja na kurahisha maendeleo yao kwa ujumla.
Nae mkazi wa
kijiji hicho Asha Nalamba amesema kuwa amefurahishwa na kitendo cha Serikali
kupeleka mradi huo vijijini na tayari ameanza kujipanga kuezeka nyumba yake kwa
bati ili aweze kunufaika na umeme huo.
"Mimi nina
nyumba ya nyasi lakini tulivyotangaziwa mradi huu, nikaanza polepole kujipanga
na mpaka sasa nimeshanunua mabati ishirini, natarajia mwezi Novemba mwaka huu kuzeeka," amesema Nalamba.
Hii ni kati ya
miradi ambayo wananchi wa Lindi na Mtwara wamepata punguzo la bei ya umeme
ambapo kwa sasa wanalipia elfu tisini na tisa tu badala ya laki nne na elfu
hamsini na tano na mwisho wa punguzo hili ni mwezi Desemba mwaka huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...