Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania katika kukuza Uimara Na kujenga Uhuru wa Vyombo vya habari na Waandishi wa Habari unatoa mafunzo kwa kwa Waandishi na wamiliki wa vyombo hivyo Mkoani Lindi ili kuwajengea Uwezo wa kuomba Ruzuku zinazotolewa na Mfuko huo
Mafunzo hayo ya Siku moja yanawezeshwa na Mshauri wa mambo ya Habari ambae pia ni mwandishi Mkongwe,Bw Ndimara Tegambwage (pichani juu) na Meneja wa Vyombo vya Habari vya SJMC Chini ya Chuo kikuu cha DSM,Bi Edda Sanga.
Kufuatia awamu ya pili ya Utoaji Ruzuku hizo toka TMF,Mfuko umeamua kutoa mafunzo hayo ili kutoa msisitizo katika Uandishi wa Habari za Vijijini,Uwazi na Uwajibikaji,Utawala bora,Ukimwi,Jinsia na kuwapa sauti za jamii zilizotengwa ili waandishi waweze kupata habari kwa jamii na habari zinazogusa jamii
Katika Mafunzo hayo pamoja na kuwezesha na wakongwe wa habari pia yamehusisha wanahabari na wamiliki toka mkoani humo yanayoweshwa na Afisa Mwandamizi wa TMF,Alex Kanyambo,Afisa Mawasiliano TMF,Japhet Sanga na Bi Raziah Mawanga,,,Afisa Mafunzo Tmf
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...