Na Baraka wa Chibiriti
Habari za majukumu Mkuu Michuzi.
Na habari zenu wadau wote!
Ambrosi Andrea Michael, ni mwanariadha wa Dodoma, anayechipukia. Ambrosi alichukua uamzi wa kukimbia kutoka Mkoa wa Dodoma hadi Mkoa wa Shinyanga kwa mguu. Na mpaka sasa alikuwa yupo mitaa ya Nzega, akiendeleza libeneke lake la kukimbia kwa miguu, kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Ambapo kilele chake kitafanyika Mkoani Shinyanga mnamo tarehe 14/10. Kutakuwa na uzimaji wa Mwenge pia. Ambrosi alikabidhiwa bendera ya Taifa Dodoma na Mkuu wa Mkoa Dodoma, na anatakiwa kuikabidhi huko Shinyanga katika kilele hicho.
Nilikutana na kuongea na Ambrosi siku moja kabla ya kuanza mbio hizo, mimi binafsi niliogopa maana ni safari ndefu sana na yenye kuogopesha hasa kukatiza misitu mikubwa, nilimwuliza kama ana uhakika kweli? Yeye alinijibu amedhamilia haswaaaa!!! Kumwenzi Baba wa Taifa kwa kukimbia, hivyo basi kaamua kwa moyo wote. Na anatakiwa kuwasili siku hiyo ya tarehe 14/10 ambayo ni siku ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa.
Nimewasiliana nae kwa njia ya simu mara kwa mara, ameniambia kwakweli amepata mapokezi na huduma nzuri sana, vituo ambavyo alipangiwa, kulala, kupumzika, kutembelea wagonjwa na kuongea na vijana chipukizi wa mambo ya michezo. Mpaka sasa anaendelea vizuri sana na hizo mbio zake.
Na mtu yoyote ambaye anapenda kuongea naye moja kwa moja kwa kumpongeza au kumchangia huduma yoyote ile anakaribishwa, kwa kupitia namba yake mwenyewe Ambrosi: 0758-004704.
Hongera Ambrosi. Kila kheri.
ReplyDeleteMuamko wa Uzalendo kama huu wa Ndugu Ambrosi ni muhimu sana kwetu nchini Tanzania mabako matumaini yamepotea kabisa!
ReplyDeleteKama mnavyoona imebaki kulaumiana tu badala ya kushirikiana na kutafuta suluhu za kupata Dira,Mwelekeo na njia za kutatua matatizo yetu.