WAISLAM JIJINI DAR WAMEANZA MAANDAMANO MCHANA HUU KUTOKEA KATIKA MISIKITI MBALI MBALI ILIYOPO KATIKA MAENEO YAO.

ASKARI WA JESHI LA POLISI WAMETANDA KILA KONA YA JIJI LA DAR ILI KUZUIA KUFANYIKA KWA MAANDAMANO HAYO,YENYE KUTAKA KUACHIWA HURU KWA BAADHI YA WAISLAM,AKIWEPO KATIBU WA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM NCHINI,SHEIKH ISSA PONDA WANAOSHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA MAKOSA MBALI MBALI YAKIWEPO YA UCHOCHEZI WA UDINI.

KATIKA MAENEO YA KARIAKOO,HALI IMEANZA KUWA TETE KWANI VURUGU NI KUBWA SANA HIVI SASA KATI YA ASKARI POLISI NA WAISLAM HAO.

GLOBU YA JAMII INAENDELEA KUFUATILIA KWA UKARIBU HALI HIYO NA ITAENDELEA KUKUPA TAARIFA KADRI ZITAKAVYOKUWA ZINAPATIKANA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. WAISLAM WANATUMIWA MASKINI LKN HAWAJIJUI! NAWASHAURI WAKAE CHINI WATAFAKARI KABLA HAWAJAFANYA KITU CHOCHOTE.....

    ReplyDelete
  2. nadhani hawa waislamu wenzangu tungeitumia fursa ya elimu tusingefika huku. Shetani anatutumia sana ila piwa kuwepo nyua kielimu kunatuangusha sana. Mwenyezi Mungu atuepushe na mabalaa

    ReplyDelete
  3. Hawa sio waiislaamu. Hawa ni wahuni wana tumia jina ya kiislam kufanya vurugu na kuharibu amani nchini.

    ReplyDelete
  4. huu ni kutokua na shughuli za msingi za kufanya...wote wanaoandamana hapo utaona ni watu wa hali ya chini tu..jamani haya mabo hayana hata faida,,hebu tujiulize amani ikitoweka kwa sisi watanzania maskini tutkimbilia wapi??,hebu tufikirie kwanza kabla ya kuipoteza hii amani enyi watanzania maskini...

    ReplyDelete
  5. hadi tuuane kama walivyouana Warundi na Warwanda ambao mauanaji yao yalikuwa ya kikabila wakati yetu sisi Watanzania yatakuwa ya kidini ambayo yote hayo kwa pamoja suluhu zake huwa hazipatikani kirahisi na huchukua miaka mingi sana mpaka baada ya watu kwishauana malaki kwa malaki kama si mamilioni kwa mamilioni.

    ReplyDelete
  6. imagine seriksali ingekuw iko chini ya mkristu ingekuwaje, maana hapo mwenzao kawajaza waislam kibao ila bado walalamika, ukweli ni kwamba shule yawasumbua

    ReplyDelete
  7. Anoy wa tatu nakuunga mkono hao sio waislamu ni wahuni wachache wanatumia jina la Dini yetu kuvuruga amani shehe Ponda na kikundi chako mshindwe na mlegee

    ReplyDelete
  8. judge you will be judged, ufumbuzi wa swala hili ni kuweka ajira kwa vijana wetu, siyo kuwaita wahuni, kwanza tungejuwa maana ya ( uhuni au wahuni ) sina kamusi hapa karibu lakini ninavyolijuwa neno hili, maana yake ni= mhuni ni mtu anayejipatia mali kwa udanganyifu sawa na tapeli kwa kiswahili kipya, au mhuni ni yule anayetenda mambo ya uasherati, awe mwanamuke au mwanaume. Sasa hawa vijana wanaoandamana,neno ( wahuni ) linawahusu kweli ?? hebu tutafuteni dawa na chanzo cha hizi vurugu, siyo kutoa majibu ya haraka haraka yasiyokuwa na solution ya kudumu, tutaanza kuiona dini ya kiislamu ni mbaya, kumbe siyo dini ila kuna baadhi ya mizizi mibovu inayoota na kusababisha mti wote kutoa matunda machungu, dawa nikuutafuta huo mzizi na kuukata -it is that simple. ma-girl friend zangu wengi ni waislam, mbona sina matatizo nao ? na sijawaona kwenye maandamano, please people ,uislam haufundishi vurugu-ni dini moja fresh kabisa na yenye masharti magumu. Zebedayo msema kweli.

    ReplyDelete
  9. naona sasa tanznia inataka kuwa kama nigeria UDINI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...