Leo katika pita pita zangu,nikabahatika kukatiza njia hii Kinondoni karibu kabisa na Bar maarufu mjini ya Mango Garden.lakini cha ajabu nilichokiona ni hii hali ya kupangwa mawe na matairi katikati ya barabara,sijui hili ni wazo la nani na alimaanisha nini??

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. City wamegoma kuweka speed bumps, wananchi wana improvise! Ukipita hapo lazma upunguze mwendo kukwepa hayo "majabali"...

    $D

    ReplyDelete
  2. HUJUI KUNA UAMSHO?

    ReplyDelete
  3. Haahaha! Mdau hapo juu umenivunja mbavu. I love my Africa,watu very creative.

    ReplyDelete

  4. Hii ni kuonyesha kuwa serikali haifanyi kazi. watu wanatumia nguvu ku-enforce law and order.

    when a government is asleep, or in leave, there means and ways the society tackle their issues!

    Poleni wana mango garden

    ReplyDelete
  5. mkijengewa barabara nzuri mnatugongea watoto,speed mpaka mwisho tufanyeje sasa hiyo ndio hali

    ReplyDelete
  6. Hii inakuwa kama kule Italia hasa maeneo ya Kusini mwa nchi ambako kwa kuwa Serikali za Manispaa ziko Likizo hivyo ''SERIKALI ZA KIUKOO ZA KIMAFIA'' ZINASHIKA NAFASI KUSIMAMIA MAMBO!

    ReplyDelete
  7. Au inakjuwa ni njia ya kuwa;punguza spidi wanendeshaji ili kuvamiwa kukabwa na kuporwa?

    ReplyDelete
  8. Au inakjuwa ni njia ya kuwapuguza spidi wanendeshaji ili kuvamiwa kukabwa na kuporwa?

    Hiyo staili ipo nchi za Amerika ya Kusini huko Brazili na Colombia Majambazi wa Mitaani hasa nje ya miji wanajenga vizuizi vya barabara au hata kutumia kamba kuwazingira waendesha vyombo vya moto barabarani na kuwafanyia uhalifu!

    ReplyDelete
  9. Au inakjuwa ni njia ya kuwapuguza spidi wanendeshaji ili kuvamiwa kukabwa na kuporwa?

    Hiyo staili ipo nchi za Amerika ya Kusini huko Brazili na Colombia Majambazi wa Mitaani hasa nje ya miji wanajenga vizuizi vya barabara au hata kutumia kamba kuwazingira waendesha vyombo vya moto barabarani na kuwafanyia uhalifu!

    ReplyDelete
  10. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kipindi cha nyuma Mateo Qaress aliwahi kupangiwa mawe barabarani nje ya mji huko Mbeya, alipokuwa akienda Kijijini aliona mawe yamepangwa alipokaribia na Dereva wake kupunguza mwendo aliona watu wanajitokeza majanini kuja na silaha za mapanga na mawe hata hivyo Mkuu wa Mkoa alikuwa na Bastola alitoa cha moto na kuanza kurusha risasi juu huku Wanyampala wakisambaa na kurudi huko Manyasiani walikotokea!

    ReplyDelete
  11. Hao Government ndiyo wanaopita na magari speed hapo? Si wananchi kama nyie, sasa hamuwezi kufuata sheria mpaka hao Government wawalazimishe?

    ReplyDelete
  12. Sawa ila je tunaopita usiku, tutaona kweli hayo mawe au tutaishia kupata ajali mbaya?????..Mbona mitaa ya kwetu tunaweka miti ya minazi tunaichimbia chini na kuipaka rangi inakuwa kama bumps???? fikirieni na usalama wa wenye magari pia, sio kufikiria usalama wa mwenda kwa miguu tu. Lets not be selfish

    ReplyDelete
  13. Acha domo wewe na serikali ya mtaa mmechukua hatua gani. Hujui wewe ni sehemu ya serikali. Bongolala!

    ReplyDelete
  14. Nakubaliana na wakazi wa eneo hili. Asilimia 90 ya madereva Dar es Salaam ni wajinga wasiojali usalama wa watu wengine. Bila kuweka vizuizi sehemu kama hii watu watakuwa wanagongwa kila siku.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...