Maelefu ya wananchi wa Mwanza wakiwa wamefurika katika uwanja wa Nyamagani jijini Mwanza leo kuuaga mwili wa aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa huo aliyeuwawa kwa kuopigwa risasi majuzi Hayati Liberatus Barlow. Mwili huo umesafirishwa kuelekea Dar es salaam ambako ataagwa na ndugu, jamaa na marafiki nyumbani kwa marehemu Ukonga kabla ya kusafirishwa kuelekea Moshi kwa mazishi.
Jeneza lenye mwili wa Hayati Kamanda Liberatus Barlow
Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Mwanza mjini wa zamani Mhe Lawrence Masha akitoa heshima zake za mwisho kwa Kamanda Barlow.





poleni sana wafiwa inasikitisha sana jinsi matukio ya kinyama yanavyoendelea nchini tanzania nchi amabayo ina sifa ya amani na upendo
ReplyDeletewingi wa watu umejionyesha namna gani marehemu alikuwa karibu sana na watu na inaonyesha jinsi huzuni zilizojaa katika nyuso za watu na kusikitishwa na tukio la kinyama kama hilo
R.I.P kamanda.