Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia alipofungua Mkutano wa kwanza wa  Kimataifa wa Kutangaza Utalii kwa Nchi za Bara la Afrika na Kuhamasisha Utalii Endelevu katika nchi hizo. Mkutano huo umefunguliwa leo Oktoba 15, 2012 katika Ukumbi wa AICC  leo Oktoba 15 Jijini Arusha na kuhudhuriwa na mawaziri 17 kutoka nchi mbalimbali za Afrika. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) akipokea barua ya wazi kutoka kwa Katibu wa Mkuu wa Shirika la Utalii la Dunia, Taleb Rifai, iliyotolewa na Baraza la Waendesha Utalii Duniani (WTTC) mara baada ya kufungua Mkutano wa Kuhamasisha utalii barani Afrika leo, Oktoba 15, 2012, jijini Arusha. Katika Mkutano huo pia umehudhuriwa na Mawaziri 17 kutoka nchi mbalimbali za Afrika

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wasanii wa ngoma ya asili wa kabila la kimasai wakati akiondoka katika ukumbi wa mikutano wa AICC jijini Arusha leo Oktoba 15, 2012 baada ya kufungua mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa Kutangaza Utalii kwa Nchi za Bara la Afrika na Kuhamasisha Utalii Endelevu katika nchi hizo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtaalam wa Tiba za Asili, James Kangaa, wakati Makamu alipokuwa akitembelea Mabanda ya Maonyesho baada ya kufungua mkutano wa kwanza wa  Kimataifa wa Kutangaza Utalii kwa Nchi za Bara la Afrika na Kuhamasisha Utalii Endelevu katika nchi hizo. Mkutano huo umefanyika leo Oktoba 15, 2012 jijini Arusha. Picha na OMR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hao wamasai wanafanya kazi kubwa sana ya kujitolea kulitangaza taifa letu la tanzania kitalii

    wakati wamasai wakijitolea kulitangaza taifa na viongozi wetu wanajitahidi kulitangaza taifa kwa ufisadi kutembelea migari ya thamani kiasi hata viongozi wa ughaibuni wanashangaa

    hao wamasai sijui hata wanathaminiwa vipi kwa taifa na wanapewa msaada gani kwa jitihada zao za kulitangaza taifa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...