Katika kusherekea wiki ya upataji nafuu yaani (Recovey week) kulifanyika mechi ya mpira wa miguu baina ya watumiaji waliopata nafuu kutoka Zanzibar (Zanzibar Sober House) pamoja na wapataji nafuu kutoka Tanzania bara.
Lengo la mechi hii lilikuwa ni kuwaweka pamoja vijana walioachana na matumizi ya dawa za kulevya na kuimarisha undugu miungoni mwao.Mechi hii ilifanyika katika viwanja vya Karume na mpaka mwisho Zanzibar Sober House walipata goli tatu na Timu kutoka bara haikupata kitu.
Mabao ya Zanzibar yaliwekwa kimiani na wachezaji Juned Abdulkadil, Tahiri pamoja na Humud (Fido).
Mechi hii ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya Sober House Recovery Art ambayo yatafanyika katika ukumbi wa Alliance Francaise Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kuanzia tarehe 17/10 mpaka tarehe 19/10/2012 kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa kumi na mbili jioni.
Ufunguzi rasmi utakuwa siku ya tarehe 17/10/2012 saa 12:30 jioni ambapo tunatarajia kuwa na wageni mbalimbali akiwemo Balozi wa Marekani, Ufaransa, pamoja na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Ndugu Suleiman Mauly (0782 000426) au Ndg Alois Ngonyani (0713 334423)
Timu ya wapataji nafuu Kutoka Bara
Timu ya wapataji nafuu kutoka zanziba
Timu zikiwa katika picha ya Pamoja


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...