Mtoto
Rashid Athumani Hamisi (12) pichani, amepotea katika mazingira ya
kutatanisha baada ya kutoweka nyumbani kwao Kiwalani Minazi Mirefu
anakoishi na Bibi yake Bi. Zamoyoni.
Rashidi
ni mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi kisutu jijini Dar
es Salaam. Tunaomba msaada wa jamii, mtu yeyote atakayemuona atoe
taarifa katika kituo cha polisi Kiwalani Minazi Mirefu au katika msikiti
wa eneo hilo.
Pia kwa mawasiliano ya simu 0713972201, 0783165655, 0762944781 na 0784531188. Rashid ni mtoto wa Mhariri wa Picha wa kampuni ya magazeti ya TSN, Athumani Hamisi, aliyepata ajali ya gari 2008.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...