Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Angela
Kairuki akiwasalimia Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakati alipofanya
ziara ya kikazi leo katika Gereza la Keko lililopo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Angela
Kairuki akionja chakula cha Mahabusu na Wafungwa wa Gereza la Keko lililopo
jijini Dar es Salaam alipotembelea sehemu ya jiko la Mahabusu na Wafungwa gerezani
hapo leo.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma
Malewa akimkaribisha Naibu wa Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Angela
Kairuki (wa pili kushoto) azungumze na Maofisa wa Magereza katika ziara ya Kikazi
aliyoifanya leo Gereza la Keko lililopo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Angela
Kairuki akizungumza na Mahabusu na Wafungwa (hawapo pichani) wa Gereza la Keko
jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kikazi gerezani hapo leo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...