Picture
 Pichani kulia ni Mkurugenzi wa makosa ya Jinai Nchini (DCI) Robert Manumbaa akiyataja majina ya watuhumiwa hao wa mauaji ya Kamanda Barlow. Kushoto ni IGP Said Mwema.
JESHI la Polisi limewataja watuhumiwa 10, na bado linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine, ambao inadai walishiriki kumuua aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow.




Kati ya watu hao watano wametiwa mbaroni Mwanza  na watu watano kutoka Dar es Salaam. Leo (jana) mjini Mwanza, mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania IGP Said Mwema, Mkurugenzi wa makosa ya Jinai Nchini (DCI) Robert Manumba aliwataja watuhumiwa  hao ni Muganizi Michael Peter (36) mkazi wa Isamilo ambaye inadaiwa alikiri mwenyewe kumuua kamanda kwa risasi.


Wengine ni Chacha Waitara Mwita (50), Magige Mwita Marwa, Bugazi Edward Kusota na Bhoke Mara Mwita (42) ambao walikamatwa jijini Dar es Salaam baada ya kuwekewa mtego kwa msaada wa wananchi.


Wanaoshikiliwa jijini Mwanza kwa mahojiano ni pamoja na Mwalimu Doroth Moses Lyimo aliyekuwa na RPC wakati mauaji yakitokea, Felix Felician Minde (50), Philemon Felician (46) maarufu kama Fumo, Bahati Agustino Lazaro (28) na Amos Magoto (30) maarufu kama Bonge.


Manumba amesema simu iliyoporwa ya mwanamama ambaye alikuwa akisindikizwa nyumbani na marehemu, ndiyo imesaidia kukamilisha upelelezi huo na hatimaye wahusika kukamatwa.


Alisema Kikosi kazi cha upelelezi kilichokuwa chini yake  Manumba kilijigawa kwenye makundi matatu moja ni lile la Ukamataji, Mahojiano na lingine la interejensia huku wakitumia njia ya sanyansi kwa kufuatia mitandao ya simu.


Marehemu Kamanda Barlow aliuawa  usiku wa Oktoba 12 majira ya kati ya saa 7 na 8 usiku katika eneo la Mianzi Mitatu, Kitangiri, kona ya Bwiru baada ya kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, wakati alipopita kumsindikiza Mwalimu Dorothy Moses nyumbani kwake kutoka katika kikao cha harusi kilichofanyika Mtaa wa Rufiji. 
Habari zaidi Bofya Hapa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Teknolojia imerahisisha kazi kwa kiwango kikubwa.

    ReplyDelete
  2. Tupeni basi na majina ya waliohusika kumteka na kumuumiza Dr. Ulimboka!!!!!

    ReplyDelete
  3. Eti njia za kisayansi, mbona kuna mengi tu ambayo mpaka leo kimyaaa hiyo sayansi yenu hamuitumii? Au hayawahusu?

    ReplyDelete
  4. UKABILA! UKABILA!! Watanzania sasa tunafahamiana kwa UKABILA, UKABILA

    ReplyDelete
  5. fasta hivi tayari mmeshawajua...duuh! akuwahusu, mnafanya kazi fasta na kwa umakini...asipowahusu mnanatanata sana na haki haitendeki.

    ReplyDelete
  6. HONGERA SANA DCI KWA KAZI KUBWA MLIYOIFANYA.MMETUPA MOYO WANANCHI.HAO WAUAJI WAUWAWE HADHARANI NYAMAGANA,KWANI ALIYEUA KWA UPANGA NAYE AUWAWE KWA UPANGA.WE SHOULD NOT NEGOTIATE WITH CRIMINALS.TUIGE MFANO WA KENYA.UJAMBAZI UMEPUNGUA KWA KIWANGO KIKUBWA,NA CHOKORAA HAWAPO TENA BARABARANI.

    ReplyDelete
  7. Sio mchezo ama kweli POLISI NGUNGURI!

    Ameuwawa mwenzenu ndani ya siku 7 tu wahalifu woooote mkononi lakini angekuwa mwananchi marehemu nadhani mngekuwa bado mnawatafuta wauwaji!

    ReplyDelete
  8. Wote wamepatikana!

    enhhh chezea Polisi weye?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...