Na Veronica Kazimoto – MAELEZO

Sikukuu ya Eid-El-Hajj itakuwa siku ya tarehe 26 Ockoba mwaka huu ambapo kitaifa swala itafanyika katika msikiti wa Vuchama, wilayani Mwanga, katika mkoa wa Kilimanjaro, ikifuatiwa na Baraza la Eid baada ya Swala.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa habari na mawasiliano ya Umma Simba Shabani wa Baraza Kuu la Waislam wa Tanzania (BAKWATA) mgeni rasmi anatarajiwa kuwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa sababu ya tarehe hiyo ni kutokana na siku hii ya leo kuwa mwezi pili, Dhul-Hijja mwaka 1433 kwa mujibu wa kalenda ya Kiislam.

Aidha Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Issa Bin Shaaban Simba amewataka Waislam wote nchini kusherehekea kwa amani na utulivu sikukuu hiyo huku wakichunga mipaka ya Allah (S.W).

Sheikh Shaaban Simba pia amewataka waislamu kutii sheria za nchi na kuepukana na watu ambao wanataka keleta tafrani za kidini hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Vuchama Ugweno au,maana Mwanga kuna Vuchama ya Ndambwe.
    Tunaomba ufafanuzi.

    ReplyDelete
  2. Eid inatarajiwa kuswaliwa hiyo Ijumaa ijayo 26 Oktoba wakati Waislamu wakiwa Lupango na wengine hawajulikani walipo!

    Hivi tunakwenda wapi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...