Viwanja vya ufukweni beach vinauzwa, zipo heka 3 Gezaulole karibu na Bamba beach ml.450,Zipi heka 10 karibu na kiwanda cha Cement Kimbiji Kigamboni ml. 200.Pia kuna shamba heka 100 Buyuni-Kigamboni ml.700.Heka 4 karibu na dar es salaam zoo sh ml.35.Viwanja vyote vina hati.Pia kuna viwanja vya ml.7 na 8 pamoja na mil.10.

Kwa mawasiliano piga simu no. 0652-020343. wekeza kwenye ardhi kwa maisha bora.
Asante.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Mdau wa Viwanja vya Ufukweni.

    Kwa bei za idadi hiyo ya hayo 'masifuri' sio kwa sisi akina 'Andolile Anyosisye Mwakabinga' watafute Mawaziri waliofukuzwa kazi ndio watamudu manunuzi!

    ReplyDelete
  2. Mdau muuza viwanja matangazo haya nakushauri uyaelekeze kwenye Mamlaka na Idara ambazo kuna hati hati watapunguzwa Watumishi!

    Ni wazi watahitaji kujiimarisha kimaisha kwa kununua viwanja kwa mapesa waliyoiba baada ya kumwagwa ktk ajira!

    ReplyDelete
  3. Haaaa!

    Moyo unapasuka kuona mapesa ya hizo bei, hivi hawa wenzetu wenye hizo fedha wanapata wapi?

    ReplyDelete
  4. Hakikisheni mumewacha mita 60 kutoka high water mark (ufukwe).

    Hii ni kwa mujibu wa sheria ya mazingira. Usipowacha ukija kuvunjiwa usilaumu.

    ReplyDelete
  5. kama kipo kiwanja cha karibu na hiyo bahari au ziwa lolote tafadhali hebu nijulishe haraka mimi nahitaji cha ujenzi wa nyumba ya kawaida tu na bei elfu sabini mpaka laki moja hivi mimi niko tayari.
    unaweza kuwasiliana na mimi haraka kwa simu hii.0783578321 au pobox 15005 daresalaam.
    asante
    mdau
    k,kitabairuka.

    ReplyDelete
  6. hawa ni wajanja wa mijini kazi yao kuzungusha. Wao wakati wanapewa hivyo viwanja kutoka mamlaka husika waliuziwa bei ya kawaida kama ziliovyoredheshwa ktk mwongozo wa utoaji viwanja/ vitalu kataki maeneo husika sasa wao wakajilikimbizia hivyo viwanja. Leo wameshindwa kuviendeleza ndio maana wanataka kuwamwagia mchanga wa macho wabongo...Hata miji ambayo imeendelea na miundo mbinu muhimu huwezi kuona upangaji mbovu wa bei za viwanja kama bongo..Hivi kweli bongo tuna upungufu mkubwa wa viwanja mpaka bei ziwe juu hivyo? MAFISADI hao..

    ReplyDelete
  7. Guys! sio wamiliki au madalali wanaopandisha bei, Ni nguvu za soko "Market Force" wanapandisha kwa maana kwa Bei hizo vinauzika. Wakulaumu serikali kwa kutozuia mfumuko wa bei kwenye ardhi. Uhitaji pamoja na mfumuko wa bei ndio vinavyopandisha bei.Vya laki tano vipo pia lakini pale sisi masikini tunapotaka kuishi standard za wenye nazo tunaishia kulaumu badala ya kutafakari. Tunalaumu sisi watatu, 10 washampigia kuulizia kuhusu hizo plot. great percent of those who acess this blog wanajiweza, Its strategically good thing.

    ReplyDelete
  8. Tsunami je? Au huko ufukweni hakuna tsunami.

    ReplyDelete
  9. Wanunuzi kabla hamjanunua viwanja hivyo tafadhalini kwanza wasiliana na ofisi ya serikali ya kijiji au ofisi ya katibu mtendaji Kimbiji,hili ujue uhalali wa umiliki wa muuzaji,pia mnashauliwa kuwasiliana na uongozi wa kijiji kimbiji,Diwani simu namba 0713768082, Mwenyekiti simu 0713846688 viongozi wa kijiji wanayajua vema maeneo na wamiliki halali wa maeneo haya

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...