Uongozi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) unasikitika kutangaza kifo cha AFISA HABARI WAKE bibi Caroline W. Manoni, kilichotokea tarehe 20/10/2012 katika hospitali ya Aga Khan, Dar Es Salaam.
maandalizi ya mazishi na msiba yanafanyika nyumbani kwa marehemu Mbezi beach karibu a msikiti wa Akram/ nyuma ya ambrosia restaurant.
maandalizi ya mazishi na msiba yanafanyika nyumbani kwa marehemu Mbezi beach karibu a msikiti wa Akram/ nyuma ya ambrosia restaurant.
Taarifa ziwafikie wafanyakazi wa wote wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), wafanyakazi wa Tanga Cement popote walipo, familia yote ya Madafa, familia yote ya Manoni na ukoo wa Uduhe, popote pale walipo
Mazishi yatafanyika siku ya jummanne tarehe 23 Oktoba 2012, katika makaburi ya kinondoni saa 9.00 mchana baada ya Misa itakayofanyika katika kanisa katoliki Mt. GAPER DEL BUFFALO MBEZI BEACH SAA 7.30 MCHANA.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa,
Bwana ametoa, Bwana ametwaa,
Jina la Bwana Lihimidiwe.
AMEN



Poleni na msiba.
ReplyDeleteTEA na taasisi nyingine za kiserikali au binafsi, siku nyingine epukeni kauli za kidini mnapotoa taarifa rasmi za msiba.
Ni taarifa gani hapo ya kidini iliyotolewa. Una matatizo mazito mdau! Hivi kwanini uwelewa wenu huwa ni mdogo?!
ReplyDeleteWe Mdau nr. 1 sijakuelewa unaposema kwamba sikunyingine waepuke kauli za kidini. Ni sehemu ina kauli ya kidi? Nisaidie labda sikielewi ninachokisoma.
ReplyDeletePoleni sana wafiwa.
Mdau namba moja nimerudi na nanukuu kifungu kinachonitatiza kama ifuatavyo:-
ReplyDeleteBwana ametoa, Bwana ametwaa
Jina la Bwana Lihimidiwe.
AMEN
wewe mdau wa kwanza acha mambo yako ya udini..sasa watu kusema kuwa bwana ametoa, bwana ametwaa tatizo liko wapi hasa ? mpaka suala la mazishi wewe unaleta mambo ya ufala na udini usio na mpango..polen sana wafiwa kwa msiba wa ndugu yenu..BWANA AMETOA, BWANA AMECHUKUA !!
ReplyDeleteSasa mbona kiarabu ni Innah Allah wa inna Illaihi Rajiun,maana ni sawa dini zote jamani jazba za nini Mungu ni moja wa sisi sote ni watoto wake.
ReplyDeleteMdau #1. na wengine kama yeye ni wa kupuuza. hawa ukiwaendekeza unapoteza muda bila sababu. waache wajifunze kwa kupuuzwa!
ReplyDeleteHuyu mdau wa 2.09 anaqute kiarabu lakini sio Inna Allah (tafsiri yake ni "Sisi ni Allah"). sahihi ni Innaa Lillaah (Sisi sote twatoka kwa Mola). OK mimi sione reason ya kubishana kwa hili baina ya Mkristo na Mwislam,. Mbona zote kauli zinafanana?
ReplyDeleteMdau wa Tue Oct 23, 02:09:00 AM 2012 nakurekebisha ni INNA LILAAH WA INNA ILLAAH RAJIUN.
ReplyDeleteNdio maana mie nikasema uelewa wa wenzetu ni mdogo.Wanahitaji kuombewa kwa Mungu ili busara iwe inatumika zaidi. Ona alivyorudi kwa nguvu zote 'ati mdau namba 1 nimerudi' halafu ananukuu pumba! Kusema Bwana ametoa na Bwana ametwaa ndio dini? Asante mdau uliemwelewesha kuwa hicho ni kiswahili tu na kuna kiarabu chake. Next time tutamwndikia kwa kiarabu. Baadala ya kucomment mambo ya maana umekalia upuuzi! Roho ya marehemu ilale pema peponi!
ReplyDelete