Uongozi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) unasikitika  kutangaza kifo cha AFISA HABARI WAKE  bibi Caroline W. Manoni, kilichotokea tarehe 20/10/2012 katika hospitali ya Aga Khan, Dar Es Salaam.

maandalizi ya mazishi na  msiba yanafanyika nyumbani kwa marehemu   Mbezi beach karibu a msikiti wa Akram/ nyuma ya ambrosia restaurant.
Taarifa ziwafikie wafanyakazi wa wote wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), wafanyakazi wa Tanga Cement popote walipo, familia yote ya Madafa, familia yote ya Manoni na ukoo wa Uduhe, popote pale walipo

Mazishi yatafanyika siku ya jummanne tarehe  23 Oktoba 2012, katika makaburi ya kinondoni saa 9.00 mchana baada ya Misa itakayofanyika katika kanisa katoliki Mt. GAPER DEL BUFFALO MBEZI BEACH  SAA 7.30 MCHANA.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa,

Jina la Bwana Lihimidiwe.

AMEN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Poleni na msiba.
    TEA na taasisi nyingine za kiserikali au binafsi, siku nyingine epukeni kauli za kidini mnapotoa taarifa rasmi za msiba.

    ReplyDelete
  2. Ni taarifa gani hapo ya kidini iliyotolewa. Una matatizo mazito mdau! Hivi kwanini uwelewa wenu huwa ni mdogo?!

    ReplyDelete
  3. We Mdau nr. 1 sijakuelewa unaposema kwamba sikunyingine waepuke kauli za kidini. Ni sehemu ina kauli ya kidi? Nisaidie labda sikielewi ninachokisoma.

    Poleni sana wafiwa.

    ReplyDelete
  4. Mdau namba moja nimerudi na nanukuu kifungu kinachonitatiza kama ifuatavyo:-

    Bwana ametoa, Bwana ametwaa
    Jina la Bwana Lihimidiwe.
    AMEN

    ReplyDelete
  5. wewe mdau wa kwanza acha mambo yako ya udini..sasa watu kusema kuwa bwana ametoa, bwana ametwaa tatizo liko wapi hasa ? mpaka suala la mazishi wewe unaleta mambo ya ufala na udini usio na mpango..polen sana wafiwa kwa msiba wa ndugu yenu..BWANA AMETOA, BWANA AMECHUKUA !!

    ReplyDelete
  6. Sasa mbona kiarabu ni Innah Allah wa inna Illaihi Rajiun,maana ni sawa dini zote jamani jazba za nini Mungu ni moja wa sisi sote ni watoto wake.

    ReplyDelete
  7. Mdau #1. na wengine kama yeye ni wa kupuuza. hawa ukiwaendekeza unapoteza muda bila sababu. waache wajifunze kwa kupuuzwa!

    ReplyDelete
  8. Huyu mdau wa 2.09 anaqute kiarabu lakini sio Inna Allah (tafsiri yake ni "Sisi ni Allah"). sahihi ni Innaa Lillaah (Sisi sote twatoka kwa Mola). OK mimi sione reason ya kubishana kwa hili baina ya Mkristo na Mwislam,. Mbona zote kauli zinafanana?

    ReplyDelete
  9. Mdau wa Tue Oct 23, 02:09:00 AM 2012 nakurekebisha ni INNA LILAAH WA INNA ILLAAH RAJIUN.

    ReplyDelete
  10. Ndio maana mie nikasema uelewa wa wenzetu ni mdogo.Wanahitaji kuombewa kwa Mungu ili busara iwe inatumika zaidi. Ona alivyorudi kwa nguvu zote 'ati mdau namba 1 nimerudi' halafu ananukuu pumba! Kusema Bwana ametoa na Bwana ametwaa ndio dini? Asante mdau uliemwelewesha kuwa hicho ni kiswahili tu na kuna kiarabu chake. Next time tutamwndikia kwa kiarabu. Baadala ya kucomment mambo ya maana umekalia upuuzi! Roho ya marehemu ilale pema peponi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...