Washiriki wa Shindano la Redd's Miss Tanzania 2012, hizi karibuni walikamilisha ziara yao ya Kutembelea Mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga kujionea vivutio vya utalii katika mikoa hiyo ambapo walimalizia mkoani Tanga kwa kutmbelea Mapango ya Amboni yaliopo mkoani humo. 

 Warembo hao wakiwa katika mapango hayo ya kale waliweza kujionea vivutio mbalimbali ambavyo ni vya kipekee na vyakuvutia vilivyopo katika mapango hayo ya asili ya zama za kale. Miongoni mwa vitu vilivyopo huko kwenye mapango hayo ni mfano wa sanamu za aina mbalimbali za Bikira Maria, Maandiko ya Quran, Daraja, sanamu za jinsia ya kike na kiume, chui, na vitu vingine mbalimbali vya kuvutia.
Warwmbo wa Redd's Miss Tanzania wakioangalia moja ya vivutio vilivyomo ndani ya Mapango ya Amboni,Jijini Tanga.hapa walikuwa wakionyeshwa mfano wa sanamu ya Mamba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...