Mtoa mada Saleh Mohammed , wa Baraza la Katiba Zanzibar akitowa mada katika mkutano wa siku moja juu ya Zanzibar katika Mchakato wa kutowa maoni ya Katiba Mpya unaoendelea Tanzania nzima,Maoni ya Katiba wiki ijayo yataaza katika Mkoa wa Mjini Magharibi , ili wananchi kupata nafasi kutowa maoni yao jinsi ya mfumo wa Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Profesa Abdul Shariff,Mwenyekiti wa Baraza la Katiba Zanzibar , akitowa mada ju ya mchakato wa kuchangia maoni ya Katiba Mpya ya Tanzania, kuhusu mfumo wa Serekali mbili za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania , wakati akitowa Elimu kwa Wananchi jinsi ya kuchangia Katiba ya Mpya ya Tanzania , Inayotarajiwa kuaza kutowa maoni yao Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi jumatatu wiki ijayo katika maeneo mbalimbali ya mjini wa Unguja.
Viongozi wa meza kuu wakifuatilia michango ya Wananchi wakati wa kutowa elimu ya mchakato wa kutowa maoni ya Katiba Mpya Tanzania.uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya bwawani ukumbi wa salama.
Wananchi wakisikiliza Mada zinazowasilisha katika mkutano wa siku moja wa kutoa elimu ya mchakato wa Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, mkutano huo umeandaliwa na Baraza la Katiba Zanzibar.iliofanyika katika ukumbi wa salama bwawani Zanzibar.
Mimi natoa maoni hapa. Mawazo yangu ni kuwa kuwe na serikali tatu. Serikali ya Tanzania, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Pemba. Serikali ya Tanzania itakuwa ni ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar ukitoa kero zote zilizokuwepo sasa kwenye muungano. Serikali ya Zanzibar itakuwa ni ile iliyoundwa baada ya mapinduzi ikijumuisha watu wa visiwa vya Unguja na Pemba. Na Serikali ya Pemba itakuwa ni ile ya watu wote wa Pemba na kujiamulia mambo yake ya ndani. Baada ya miaka kumi Serikali ya Pemba itakuwa na uhuru wa kuamua kuwa taifa kamili au kuingia kwenye muungano wa nkataba na serikali nyengine hizi mbili.
ReplyDelete