Sisi wanafunzi wa kitanzania nchini Urusi ,tunakosa huduma za msingi kama vile malazi , chakula na bima ya afya.
Serikali kupitia bodi ya mikopo ya elimu ya juu na Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi ,kwania njema iliamua kusomesha wanafunzi wa kitanzania katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Urusi.
Lakini kutokana na utendaji mbovu na ubinafsi wa baadhi ya watendaji wa Bodi ya mikopo, kumekua na ucheleweshwaji wa ulipaji wa pesa za kujikimu , malazi na bima ya afya kwa zaidi ya miezi mitatu sasa bila sababu za msingi toka kuanza kwa mwaka wa masomo 2012/13.
Hali hii imetupelekea wanafunzi kuanza kufukuzwa katika hosteli tunazoishi pamoja na kutopatiwa huduma za afya pindi tunapo ugua.Ikumbukwe kuwa katika nchi za ulaya huwezi pata matibabu kama huna bima ya afya.
Shukrani zetu za dhati ziende kwa Ubalozi wa Tanzania nchi Urusi kwa kushirikiana bega kwa bega na Wanafunzi katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili linalotukabili katika kipindi hiki kigumu pamoja na majuku mengi waliyonayo, pamoja na jitihada hizo mpaka sasa hakuna ufumbuzi wowote uliopatikana.
Tunaandika waraka huu kwa huzuni na masikitiko makubwa sana kwa sababu kutopatiwa mikopo mpaka sasa sio tu kunafanya wanafunzi waishi maisha magumu na hatari, vilevile kunatia aibu Taifa kwa kutolipa ada kwa wakati. Wengine ndo wamefika mwaka huu wako mbali kutoka moscow na hakuna mtanzania yeyote huko.... Yaani sasa wanafunzi watanzania tunajulikana na wanafunzi wengine kuwa ni watu wenye shida sana na ombaomba kwa kweli ni aibu
Tunaamini kabisa Serikali kupitia bodi ya mikopo ,wizara ya elimu na mafunzo stadi na ufundi na ubalozi wa Tanzania Nchini Urusi una nia njema kabisa kusomesha vijana wake nje ya nchi, ispokua tu kuna baadhi ya watendaji wa bodi ya mikopo wamekua wazembe na kutowajibika kwani wamekua wakitoa majibu ya uongo na jeuri kwa uongozi wa wanafunzi na maafisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Urusi.
Ombi letu kwenu ni kutufikishia ujumbe huu kwa wahusika na watendaji wa ngazi za juu za bodi ili waweze kutusaidia sisi wanafunzi wa Urusi ambao tupo hatarini huku ugenini.
Tunatumaini kutokana na Uzito wa tatizo letu wahusika watalishughurikia na kulitatua tatizo hili kwa haraka zaidi na kutupa ufafanuzi wa ucheleweshwaji wa mikopo ya wanafunzi kwa zaidi ya miezi mitatu(3).
WANAFUNZI NCHINI URUSI.
kaaaaaaaaaazi kweli kweli
ReplyDelete......maisha bora kwa kila Mtanzania. Zidumu fikra za mweyekiti na chama chake! jamani tusichokonoane,,,hela yetu ipo uswisi tunasubiri izae faida! hayo ndio maendeleo,,tulijaribu na sasa tunasonga mbele...
ReplyDeletePoleni sana ndugu zanguni...watu walikuwepo kwenye vikao vya ccm leo ndio wamemaliza, nafikiri soon pesa zitapatikana.....hili ndio tatizo la wafanyakazi wa taasisi za serikali,mawaziri,makatibu wakawa wanachaguliwa kisiasa, mkurugezi wa taasisi fulani huyu huyo ni mjumbe wa chama fulani haya mambo yanatusumbua sana watanzania....mambo haya katika katiba lazima tuyasemee.
ReplyDeletekwanini tunapeleka watu nje wakati tunajua baadhi ya watendaji wababaishaji ni aibu kwa taifa. kwa hali hii hatuwezi kuthaminika popote duniani why this
ReplyDeleteWananikumbusha machungu tuliyoyapata tukiwa ukraine chini ya hao bodi ya mikopo,binafsi nilishapelekwa mahakamani mara tatu kwa vipindi tofauti kwa kupitiliza kibali cha kuishi (student permit) kwa kutolipa ada kwa wakati muafaka,sikufungwa jela isipokua nilikua natozwa faini hivyo utwo tufedha twa bodi nilikua nagawana na uhamiaji kila wakati, kama huna kibali hutotembea kwa kuogopa askari ambao wanataarifa zote toka ktk system zao pia suala la darasa na huduma zingine za kijamii sahau, wengi waliacha shule na wengine hata kuathirika kisaikolojia na kupata magonjwa ya kuchanganyikiwa. Nashukuru binafsi nilikomaa na kumaliza kwa sasa nipo Ludwig institute of cancer ndani ya australia makamuzi kama kawa na ipo siku nitatimba bongo na naamini nitatoka tu kibingwa.komaeni washkaji napenda kuwapa ari najua ni ngumu maana nami nilikua mazingira hayohayo.
ReplyDeleteHamna bana ,sasa si mpige box mbona wa watu wa afrika magahribi wanapiga box na shule acheni ulelemama nyie !
ReplyDeleteRushwa imetawala Kila section. Kunasection zingine hazihitaji kuwa na Rushwa, Kwa kweli nilishangaa sana kusikia mtu anaye omba mkopo analazimika kutoa Rushwa Inakuwaje, mm ninaye omba huo mkopo ndio nitakaye lipa huo mkopo tena wenye intrest kubwa halafu tena nitoe rushwa Kwa huyooo aliyekaa hapo officin kuprocess huo mkopo. Tutafika kweli tuendako? Naona tunaeleka nageria. Wa tz tunatakiwa kupenda nchi yetu na kuacha kuwa ma selfish. Chukueni mfano wa Rwanda
ReplyDeleteHakuna kupiga box Russia, wenyewe wanapiga mabox nje ya nchi yao, thats Russia not UK
ReplyDeleteWatanzania mlioko nje ya nchi mmezidi kulalama. hamjui hiyo mikopo ni mpaka sisi tuliopo nchini tutozwe kodi ndio bodi wapewe?
ReplyDeleteMwangalie huyo anayeringa kuwa tumemsomesha akakimbilia australia; Je hela zetu umerudisha? hujui watu aina yako ndio wanaokwamisha marejesho ndio wengine kama hao wanaolalamika ndio wapewe?
Huko ni ugenini tu hata kuwe kuzuri vipi. Mimi nimeishi nchi nyingi ikiwa ni pamoja na hiyo Australia, Vanuatu nk. Lakini huwezi kuiponda Tanzania iliyokulea mpaka ukaona huko nje. Si ajabu mpaka sasa una Passport ya Tanzania.
Hizi diaspora zinajukumu pia la kuhimiza uzalendo.
Ulaya na Marekani wana mambo mabaya mengi lakini raia wao ni nadra kukashifu nchi zao.
Utaona watu wanasema elimu yetu hovyo wakati huo wanalalamika hawana kazi. utapataje hiyo kazi wakati umeshaimbia dunia kuwa una elimu duni? Kuweni na akili wakati mwingine. Fursa mnajikosesha kwa vinywa vyenu wenyewe?
Director of Loan recovery trace this guy and recover our money. Australian Embasy in Nairobi is the starting point.
POLENI SANA WADOGO ZANGU,TUJARIBU KUWAFUATILIA JAMAA WA LOAN BOARD
ReplyDeleteSAYS YOUR BROTHER ANDENDEKISYE
andendekisye hihi
ReplyDelete