Baraza la Famasi linapenda kutoa
ufafanuzi kwa umma kuhusu Tangazo la Chuo
Kikuu Cha Ekernforde - Tanga kuanza udahili (admission) wa wanafunzi katika
ngazi ya cheti na diploma katika pharmaceutical sciences, katika gazeti la Mwananchi
la tarehe 10 Oktoba 2012 toleo ISSN 0856-7573 Na. 04490.
Baraza la Famasi ni Taasisi ya
Serikali iliyoko chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii iliyoanzishwa chini
ya Sheria
ya Famasi Na. 1 ya 2011. Baraza hili pamoja na majukumu mengine limepewa wajibu
wa:-
1. kuhakiki na kupitisha (approval) Mafunzo na Mitaala inayohusu taaluma ya famasi nchini kwa mujibu
wa vifungu 4(i),(p) na 5(h)
2. Kuhakiki, Kusajili na kupitisha
Taasisi za Elimu na Mafunzo ya Taaluma za Famasi nchini, na
3. kusajili wataalamu wa taaluma ya
famasi nchini .
Kwa kuzingatia Sheria ya Famasi, 2011,
Baraza linapenda kutoa taarifa kwa umma kuwa Chuo Kikuu Cha Ekernforde
kilichopo Tanga Mjini hakijaidhinishwa wala kusajiliwa na Baraza na hivyo hakitambuliwi wala hakikubaliki na
Baraza kutoa mafunzo ya aina yo yote ile katika
taaluma ya dawa (certificate, diploma or bachelor in
pharmaceutical sciences). Vilevile hata mitaala yake ya kufundishia
haijaidhinishwa wala kusajiliwa wa Baraza.
Kwa Taarifa hii, Baraza
linawatahadharisha wananchi kutotumia chuo hiki kutokana na ukweli kuwa hakitambuliwi
kisheria na Baraza la Famasi kwa vile hakijawasilisha taarifa wala kusajiliwa
na Baraza. Taasisi yoyote inayokusudia
kutoa mafunzo ya dawa, ni lazima ipate
idhini ya Baraza ili wanafunzi waweze kusajiliwa pindi watakapokamilisha
mafunzo yao .
Baraza linasisitiza kuwa kutokana na
Chuo hiki kutokidhi masharti na vigezo vya Sheria, wanafunzi watakaosoma katika Chuo hiki hawatatambuliwa wala kusajiliwa na Baraza
hivyo kupoteza sifa ya kuajiriwa Serikalini,
Taasisi binafsi, na hata
kujiajiri.
Baraza linapenda kuwasisitizia
wananchi ya kuwa kabla ya kumwandikisha mtoto wako katika chuo chochote
kinachoendesha masomo ya fani ya famasi, ni muhimu mwenye chuo akuoneshe kibali
cha Baraza.
Imetolewa
na:
Msajili,
Baraza la Famasi,
S.
L. P. 31818,
Kwa
mawasiliano, Simu: 022–2451007 au 0684/0755-881677/0655881676
Duh. Tangazo halijakamilika. Haitoshi tu kutahadharisha umma. Vipi kwa ambao watasoma kwa kuwa hawakuona tangazo hili? Mnachukua hatua gani dhidi ya hicho chuo? Suala muhimu ni kuhakikisha chuo hicho hakisajiri mwanafunzi ktk fani hiyo.
ReplyDeleteKwani tatizo nini??Lazima kuna 'KITU' hapa.Busara zaidi zitumike,tatizo limalizwe,kama kuna mapungufu yapo chuo kiyatimize.Siungi mkono chuo kutoa kozi bila kukidhi mahitaji,tena kozi zenyewe za 'HATARI.
ReplyDeleteJamani sasa nifanyeje?
ReplyDeletenimeapply kwenda kusomea DIPLOMA IN CLINICAL MEDICINE NA APPLICATION zao ZILIKUWA NAMASHARTI KUWA LAZIMA UAMBATANISHE PAY SLIP YA BENKUKIWA UMEINGIZA Tsh 20000 KATIKA ACCOUNT YAO. DUH! KIUKWEKI IMENIKATA.
ILA TUNAOMBA WAKISAJIRI CHUO HIKI KUSUDI TUWEZE KUSOMA HAPO AMBAO TAYARI TUMESHA TUMA APPLICATION ZETU KATIKA CHUO HIKI.
EEEEE MUNGU TUSAIDIE WANAO.
nalo neno lakini mimi naomba principal wa chuo hiki achukue tahadhari mapema kabla mambo hayajawa makubwa hasa pindi ambapo wanachuo wanaweza wakawa wamehitimu and then serikali inasema hamna mtu yeyote aliyesoma EKERNFORD TANGA UNIVERSITY KUAJIRIWA KWENYE SECTOR ZOTE.
ReplyDelete