Baraza la Famasi linapenda kutoa ufafanuzi  kwa umma  kuhusu Tangazo la Chuo Kikuu Cha Ekernforde - Tanga kuanza udahili (admission) wa wanafunzi katika ngazi ya cheti na diploma katika pharmaceutical sciences, katika gazeti la Mwananchi la tarehe 10 Oktoba 2012 toleo ISSN 0856-7573 Na. 04490.

Baraza la Famasi ni Taasisi ya Serikali iliyoko chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Famasi Na. 1 ya 2011. Baraza hili pamoja na majukumu mengine limepewa wajibu wa:-
1.     kuhakiki na kupitisha (approval)  Mafunzo  na Mitaala  inayohusu taaluma ya famasi nchini kwa mujibu wa vifungu 4(i),(p) na 5(h)
2.     Kuhakiki, Kusajili na kupitisha Taasisi za Elimu na Mafunzo ya Taaluma za Famasi nchini, na
3.     kusajili wataalamu wa taaluma ya famasi nchini .                                                                                                       
Kwa kuzingatia Sheria ya Famasi, 2011, Baraza linapenda kutoa taarifa kwa umma kuwa Chuo Kikuu Cha Ekernforde kilichopo Tanga Mjini hakijaidhinishwa wala kusajiliwa na Baraza  na hivyo hakitambuliwi wala hakikubaliki na Baraza kutoa mafunzo ya aina yo yote ile katika   taaluma ya  dawa (certificate, diploma or bachelor in pharmaceutical sciences). Vilevile hata mitaala yake ya kufundishia haijaidhinishwa wala kusajiliwa wa Baraza.

Kwa Taarifa hii, Baraza linawatahadharisha wananchi kutotumia chuo hiki kutokana na ukweli kuwa hakitambuliwi kisheria na Baraza la Famasi kwa vile hakijawasilisha taarifa wala kusajiliwa na Baraza. Taasisi yoyote  inayokusudia  kutoa  mafunzo ya dawa, ni lazima ipate idhini ya Baraza ili wanafunzi waweze kusajiliwa pindi watakapokamilisha mafunzo yao.

Baraza linasisitiza kuwa kutokana na Chuo hiki kutokidhi masharti na vigezo vya Sheria, wanafunzi  watakaosoma katika Chuo hiki   hawatatambuliwa wala kusajiliwa na Baraza hivyo kupoteza sifa ya kuajiriwa Serikalini,  Taasisi  binafsi, na hata kujiajiri.

Baraza linapenda kuwasisitizia wananchi ya kuwa kabla ya kumwandikisha mtoto wako katika chuo chochote kinachoendesha masomo ya fani ya famasi, ni muhimu mwenye chuo akuoneshe kibali cha Baraza.
  
Imetolewa na:
Msajili, Baraza la Famasi,
S. L. P. 31818,
Dar es Salaam.
Kwa mawasiliano, Simu: 022–2451007 au 0684/0755-881677/0655881676

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Duh. Tangazo halijakamilika. Haitoshi tu kutahadharisha umma. Vipi kwa ambao watasoma kwa kuwa hawakuona tangazo hili? Mnachukua hatua gani dhidi ya hicho chuo? Suala muhimu ni kuhakikisha chuo hicho hakisajiri mwanafunzi ktk fani hiyo.

    ReplyDelete
  2. Kwani tatizo nini??Lazima kuna 'KITU' hapa.Busara zaidi zitumike,tatizo limalizwe,kama kuna mapungufu yapo chuo kiyatimize.Siungi mkono chuo kutoa kozi bila kukidhi mahitaji,tena kozi zenyewe za 'HATARI.

    ReplyDelete
  3. Jamani sasa nifanyeje?
    nimeapply kwenda kusomea DIPLOMA IN CLINICAL MEDICINE NA APPLICATION zao ZILIKUWA NAMASHARTI KUWA LAZIMA UAMBATANISHE PAY SLIP YA BENKUKIWA UMEINGIZA Tsh 20000 KATIKA ACCOUNT YAO. DUH! KIUKWEKI IMENIKATA.
    ILA TUNAOMBA WAKISAJIRI CHUO HIKI KUSUDI TUWEZE KUSOMA HAPO AMBAO TAYARI TUMESHA TUMA APPLICATION ZETU KATIKA CHUO HIKI.
    EEEEE MUNGU TUSAIDIE WANAO.

    ReplyDelete
  4. nalo neno lakini mimi naomba principal wa chuo hiki achukue tahadhari mapema kabla mambo hayajawa makubwa hasa pindi ambapo wanachuo wanaweza wakawa wamehitimu and then serikali inasema hamna mtu yeyote aliyesoma EKERNFORD TANGA UNIVERSITY KUAJIRIWA KWENYE SECTOR ZOTE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...