Wizara ya Maliasili na Utalii itaendesha zoezi la kuwaangamiza Kunguru Weusi katika Manispaa ya Morogoro kuanzia tarehe 16 Novemba hadi 15 Desemba 2012.

Kunguru weusi watauwawa kwa kutumia sumu tulivu aina ya DRC 1339 ambayo haina madhara makubwa kwa binadamu. Hata hivyo tahadhari inatolewa kuwa watoto wasichezee mizoga ya kunguru iliyoanguka barabarani na mitaani.

Wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano kwa kikosi kazi kinachoendesha zoezi hilo kwa kutoa taarifa kuhusu maeneo yenye idadi kubwa ya Kunguru weusi. Aidha, taarifa zitolewe endapo mizoga ya kunguru itaonekana katika makazi ya watu na barabarani.

Lengo la operesheni hii ni kupunguza idadi ya kunguru weusi ambao wanasababisha kero na adha kwa wananchi katika makazi yao. Pia kunguru hao wamekuwa wakiua viumbe wa asili wakiwemo ndege pamoja na kueneza vimelea vya magonjwa kama vile kuhara na mdondo kwa kuku.


Zoezi hili ambalo limeshafanyika katika Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Tanga litaendeshwa Morogoro kwa mara ya mwisho kabla ya kurudi tena Dar es Salaam kukamilisha zoezi katika sehemu ambazo zitakuwa na kunguru weusi waliosalia.


Kuanzia mwezi Julai 2010 hadi Oktoba 2012 Jumla ya kunguru weusi 856,831 wameshauawa kwa kutumia sumu hiyo ya DRC 1339 na mitego katika Jiji la Dar es salaam, Pwani na Tanga.

Katika Manispaa ya Morogoro taarifa kuhusu Kunguru Weusi zitolewe katika ofisi za Maliasili, pamoja na kupiga simu kwa: Meneja mradi – 0754498957 au 0716129120 na Mtaalamu wa sumu – 0757 – 585358.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Naunga mkono wauawe, lakini wasimalizwe. Kuwepo na kahifadhi fulani ka kuwaweka wachace kwa ajili ya mambo mbalimbali ikiwemo historia, utafiti n.k.

    ReplyDelete
  2. MNGEWAKAMATA NA KUWAUZIA UNITED STATE OF AMERICA WANAWATAKA HAO KUNGURU AU MNGEWAUZIA NCHI ZINAZOKULA KUNGURU PESA ZIPATIKANE KWA MATIBABU YA WATOTO.

    ReplyDelete
  3. Ndege mwenye akili, mithili ya binadamu!

    Atatushinda tu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...