Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Masumbwi Mohamed Chibumbuli akiwa chini huku akihesabiwa baada ya kupata kichapo kutoka kwa bondia wa Zambia Mbachi Kaonga
Wasanii wa kikundi cha Sanaa cha Zinduka Entertaiment cha Temeke wakitoa burudani kabla ya mpambano wa Zambia na Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita


Wasanii wa kikundi cha Sanaa cha Zinduka Entertaiment cha Temeke wakitoa burudani kabla ya mpambano wa Zambia na Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita

Bondia Saidi Hofu wa Tanzania kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana masumbwi na bondia Caristo bwalia wa Zambia wakati wa mpambano wao wa kirafiki wa Kimataifa uliofanyika mwishponi mwa wiki iliyopita.

Bondia Mbachi Kaonga wa Zambia kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana masumbwi na Mohamed Chimbumbui wa Tanzania Kaonga alishinda kwa point wakati wa mpambano wao wa kirafiki wa Kimataifa uliofanyika mwishponi mwa wiki iliyopita picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Meneja Mwendeshaji wa Kampuni ya Joker Club Olec Aleksejev kulia akitunishiana misuri na bondia wa timu ya Taifa ya Masumbwi Said Hofu baada ya kumkabizi vifaa kwa ajili ya mchezo huo baasda ya kuibuka mcherzaji bora wa mashindano kati ya Zambia na Tanzania
  
Bondia Mohamed Chimbumbui wa Tanzania (aliyevaa nyekundu) akizuia ngumi nzito za Mbachi Kaonga wa Zambia kg 75. Picha na SuperBoxing D


MABONDIA wa ngumi za Ridhaa wa Tanzania mwishoni mwa wiki iliyopita wamechezea kichapo baada ya kupigwa michezo minne kati ya mitano iliyochezwa  na mabondia toka Zambia kwenye ukumbi wa DDC Kariakoo

Mapambano haya ambayo yalikuwa ni ya kirafiki ya kimataifa yanayojulikana na Shirikisho la ngumi za Ridhaa Duniani AIBA yenye raundi tatu ilishuhudia Said Hofu akifungua pazia (kg 49) kwa kupigwa kwa pointi na Caristo Bwalia toka Zambia

Mpambano wa pili kg 56 ulishuhudia Frank Nicolaus wa Tanzania akipigwa na Russel Mwamba wa Zambia kwa pointi pia.

Kg 60 ndipo mtanzania Ismail Galiatano alimshushia ngumi nzito nzito John Chimpwele wa Zambia na kusababisha kuchanika juu ya jicho na kutokwa damu nyingi ndipo mwamuzi alisimamisha mchezo na kumpa ushindi Ismail Galiatano.(RSC)

Mpambano wa nne kg 64 Mtanzania Kassim Hussein alipokea kipigo toka kwa  Charles Lumbwe kwa kupigwa kwa pointi.

Funga kazi kg 75 ikawa ndio usiseme maana Mohamed Chimbumbui alipigwa kwa TKO na Mbachi Kaonga wa Zambia baada ya kumsukumizia makonde mazito mazito na kushindwa kuyahimili na kujikuta akianguka kila mara.

Katibu wa Chama ngumi za ridhaa, Makore Mashaga alisema wamepoteza mpambano huo lakini anashukuru wamepata mazoezi ya kujiandaa na mashindano ya ndano yanayotarajiwa kuanza Novemba 26 kwenye uwanja wa ndani wa taifa, jijini Dar es salaam.

Mabondia watanzania walisema kupigwa kwao kunatokana na maandalizi hafifu waliyopata na mashindano kuahirishwa mara kwa mara pia kuliwafanya morali kushuka.

Naye Katibu wa Ngumi za Ridhaa wa Zambia Lut. Kanali Man Muchimba amesema amefurahi kucheza na watanzania kwani wamepata mazoezi ya kuwasaidia kucheza mashindano ya kanda ya tano yatakayofanyika nchini kwao mapema Desemba.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Enhhh Watanzania sisi ushiriki wetu Michezoni ni kwa mabishano ya Vijiweni tu.

    Si mnaona wa Zambia wanavyotu dunda?

    ReplyDelete
  2. Wazambia ngumi jiwe!

    Hawa jamaa huko kwao hawana msamiati wa neno 'chai' ni kuwa mtu akiamka asubuhi Kifungua Kinywa ni Ugali tena wa dona na Mbaazi, Kunde, Maharage au Samaki!

    Sasa kwa Mtaji huo sisi na Mabondia wetu wa chips mayai tutaweza?

    ReplyDelete
  3. Tanzania Mahindi ya Dona tunalima sisi, Zambia yeye mlaji mzuri wa Ugali!

    Hapo Madogo wetu hawa wa Ubaunsa wa kunyanyua matofali vichochoroni na kwenye Makempu Mitaani watafua dafu kweli?

    ReplyDelete
  4. Fedha ni tamu Wajameni !

    Lakini ahhh isiwe tabu yaani gumi la uzito wa Kg. 75 kutoka kwa Mbachi Kaonga wa Zambia linatua ktk shavu langu usoni mimi Maganga Bahati wa Tanzania si ndio sasa kupeana Kiharusi na kupooza mwili?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...