Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Katika na Sheria, Mhe. Mathias Chikawe, na Wahe. Majaji Wakuu kutoka Uganda na Kenya (Mhe. Benjamin Odok-Uganda na Mhe. Willy Mutunga-Kenya) pamoja na ujumbe wa Tume ya Marekebisho ya Sheria Nchini ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Jaji Mstaafu, Mhe. Joseph Sinde Warioba.
Warsha hiyo iliyofunguliwa na Mhe. Chikawe ina lengo la kutoa fursa kwa Waheshimiwa Majaji kutoa maoni yao katika mchakato mzima wa uundwaji wa katiba mpya, waliopo nyuma ni baadhi ya kundi la Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Tanzania wanaoshiriki katika warsha hiyo. Picha na Mary Gwera
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...