Wajumbe wa Baraza Kuu la 67 la Umoja wa Mataifa, wakiangalia matokeo ya kura walizopiga kuunga mkono Azimio linalotaka kuondolewa kwa Vikwazo vya kiuchumi, kibiashara na fedha ambavyo Marekani imeiweka Cuba tangu mwaka 1962.
Upigaji kura wa Azimio hilo umefanyika siku ya jumanne ikiwa ni mara ya 21 kwa nchi wanachama kupigia kura Azimio hilo. Matokeo ya kura hiyo yalikuwa, nchi 188 zilipiga kura ya ndiyo kwa maana ya kuunga mkono Azimio, nchi Tatu Marekani, Israel na Palau zilipiga kura ya hapana, huku nchi mbili Marshall Islands na Macronesia zikipiga kura ya kutofungamana na upande wowote.
Ukumbi Mkuu wa Mikutano ya Baraza Kuu ulilipuka kwa nderemo baada ya Rais wa Baraza Kuu kutangaza matokeo ya kura hizo.
Nani kasema kuna demokrasia duniani?
ReplyDeleteMarekani anaogopa wapiga kura milioni moja wa Kimarekani wenye asili ya Cuba wanaiiipinga serikali ya kimomunisti ya Cuba. Hawa wana nguvu za kura na wanaishi Miami , Florida.
Mpaka pale watakaporudishiwa mali zao na Castro zilizotaifishwa na Cuba kuwa huru tena ndio vikwazo hivi vitaondoka.
Ukieleka umuhimu wa kura zao katika siasa ya Marekani, utaelewa kwa nini vikwazo ni vigumu kuwekwa. Umoja wa Mataifa kwa Marekani sio muhimu sana kuliko kura nchini kwao na makelele yote yatashindikana tu kama miaka ya nyuma, sauti haina nguvu hapo.
ReplyDeleteWamarekani walitemeshwa biashara ya mafuta na mpaka leo Serikali ya Cuba ndiyo inasimamia biashara ya mafuta.
Cuba ilikataa wamarekani kuingia kwenye mafuta. Pia wamarekani wanahofia vikwazo vikiondolewa, warusi watakuja jenga kambi Cuba maana mafahali wawili watasogeleana sana for comfort.