Kamera ya Globu ya Jamii iliwanaswa Watoto hawa   wakivua Samaki aina ya Kambare katika Bwawa la Mwanakwerekwe,huko Zanzibar. 
Tatizo la baadhi ya Wananchi kutupa taka kwenye mitaro,husababisha hadha kubwa ya barabara kujaa maji pindi inyeshapo ndogo.hali hiyo inakuja kutokana na mitaro hiyo kuziba kutokana na taka hizo.Hapa ni katika barabara ya Kijangwani,Zanzibar.
Maendeleo ya ujenzi wa Barabara aliyoiahidi Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanzia,Mh. Benjamin Mkapa ikiendelea huko Darajabovu Zanzibar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Bwana Muhidini michuzi tunakuheshimu sana tuu lakini tunakuomba kukufahamisha kuwa Raisi wenu mstaafu mkapa hakuwahi kuwasaidia wazanzibari hata siku moja isipokuwa kuwadhalilisha na kuwaona si watu na ndio mpaka leo unatuona hapa tulipofikia kwa hiyo ikiwa huna story ya kuandika na wewe usianze kutuzalilisha kwa kutuambia bara bara alioiahidi MKAPA wadanganye hao hao WATANGANYIKA wenzako sisi wazanzibar tumeshaamka na hamutotudanganya tena. GOD BLESS ZANZIBAR.

    ReplyDelete
  2. kwa comment ya hapo juu..I must say I am one ashamed Zanzibari!!! sad, pathetic hurt!

    ReplyDelete
  3. Wewe Anonymous wa hapo juu wacha uongo au kusema kitu usichokuwa na uhakika nacho.

    Kusema ukweli wakati wa Salimini walipokuwa wanachukuwa fedha zote yeye, former MoF (lady ASA) na ndugu yake PS wa Fedha OS tulikuwa tunakwenda miezi 3 sisi wafanyakazi wa serikali bila kupata mshahara.

    Aliyetusevu alikuwa Mkapa au mumesahau sasa kwa kuwa kuna GNU?

    Musimtoe shukurani mtu kwa sababu tu hamumpendi. Munajipatia dhambi za bure.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...