Meneja
Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Peter Fauel, akitangaza Punguzo la
Asilimia Kumi ya Malipo ya mwezi kwa wateja wa Televisheni kwa Vipindi
vya DStv likaloanza hapo kesho, ambapo amesema punguzo hilo
litawawezesha wateja wao kulipia huduma za Matangazo ya Televisheni ya
kituo hicho kwa gharama nafuu. Pia amesema Offer hiyo ya Punguzo la bei
ni hatua ya Kampuni hiyo kurudisha fadhila kwa wateja wake kuelekea
katika kipindi cha maadhimisho ya sikukuu za mwisho wa mwaka. Kulia ni
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Barbara Kambogi na Kushoto ni
Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Bi. Furaha Samalu.
Meneja
Masoko wa Multichoice wa Kampuni hiyo Bi. Furaha Samalu akitoa
ufafanuzi kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea matumizi ya mfumo wa
Digitali DStv kwa kuwajali wateja wake imepunguza gharama za
kuunganishwa ambapo sasa ni kwa shilingi za Kitanzania 169,000 unaweza
kusheherekea msimu wa sikukuu na DStv.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multchoice
Barbara Kambogi (wa pili kushoto) akiwahakikishia wateja wa DStv kuwa
sasa kampuni hiyo imezidi kuboresha huduma zenye viwango vya hali ya juu
na kuwataka wazazi kutumia fursa hii ya punguzo la bei ya kuunganishwa
ili watoto wao waweze kushuhudia vipindi mbali mbali vya kuelimisha na
kuburudisha ikiwemo filamu kali, katuni maridadi, michezo mbalimbali
katika kipindi hiki cha likizo kwa watoto wao na kuwa huu ndio sasa muda
muafaka kwa kujipatia DStv.
Asanteni.Lakini bado,nendeni mbele zaidi,tunaomnba tulipie kadri tunavyoangalia kwa maana ya gharama ziwe tu pale Decorder inapokuwa inafanya kazi.Hapo kwa kweli mtakuwa mmetujali sana sisi 'WALAJI'.Kwa ufupi mko juu.
ReplyDeleteDavid V