Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akiongea na Wadau wa Sekta ya Michezo katika Kikao cha kujadili Rasimu ya Sera ya Michezo pamoja na Itifaki ya kuridhia Mkataba wa Kimataifa wa udhibiti wa matumizi ya dawa za kuongeza nguvu katika Michezo.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa kujadili Rasimu ya Sera ya Michezo wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga (Hayupo Pichani) wakati wa ufunguzi wa kujadili Rasimu ya Sera hiyo.Wa kwanza Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Ndugu Assah Mwambene.
Wadau wa Sekta ya Michezo wakiwa katika picha ya pamoja katika Mkutano wa kujadili Sera ya Michezo.Wanne Kutoka kushoto waliokaa ni mgeni rasmi Bi. Sihaba Nkinga.Mkutano huo umefanyika jana Jijini Dar es Salaam. (Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...