Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Gilles Muroto akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Ulinzi shirikishi uliofanyika katika shule ya Msingi Sokoni One iliyopo katika jiji la Arusha. mkutano huo uliofanyika tarehe 12.11.2012 uliwajumuisha askari wa jeshi la Polisi, viongozi wa kata ya Sokoni one na askari wa vikundi vya Ulinzi shirikishi.
Mkuu wa kitengo cha Polisi Jamii mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi (SP) Mary Lugola akitoa elimu ya Polisi Jamii kwa askari wa vikund vya ulinzi shirikishi katika mkutano uliofanyika shule ya Msingi Sokoni One iliyopo kata ya Sokoni One jijini Arusha juzi tarehe 12.11.2012.
Maofisa wa Jeshi la Polisi waliokaa kutoka kushoto ni Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha (SSP) Gilles Muroto, Mkuu wa kitengo cha Polisi Jamii mkoa wa Arusha (SP) Mary Lugola na Mkuu wa kituo cha Unga Limited (SSGT) Shaban Shaban wote kwa pamoja wakimpongeza kwa kumpigia makofi afisa Mtendaji wa Kata ya sokoni One Bw.Gustafu Milambo(Aliyesimama) kutokana na kazi nzuri anayeifanya kwenye kata yake juu ya uanzishwaji wa vikundi imara vya polisi Jamii.
Baadhi ya kikundi cha polisi Jamii cha mtaa wa Kanisani katika kata ya Sokoni One wakisikiliza kwa umakini elimu ya Ulinzi shirikishi iliyokuwa inatolewa na Maofisa wa Jeshi la Polisi mkoani hapa. Mkutano huo ulifanyika juzi tarehe 12.11.2012 katika shule ya Msingi Sokoni One iliyopo jijini Arusha. (Picha na Mahmoud Ahmad)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Sasa mnawaweka tena hadharani? Si mtaacha wauwawe na majambazi?

    ReplyDelete
  2. ukiwaona kama watu!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...