Mwalimu Mboya akisindikizwa na walimu wenzake wakitoa msaada wa ndala dazani moja, dawa za mswaki dazani mbili na miswaki dazani mbili. Kuanzia kushoto ni Mwalimu Ana Kimatare, Mzee Hamisi Mwakimwagile (akiyepokea msaada huo kwa niaba ya Tanzania 50 Plus Campaign), Mwalimu Florence Mboya, Mwalimu Happy Lumbwe na Mwalimu Ng’walu Mipawa.
Tanzania 50 Plus Campaign ikishirikiana
na waathirika wa saratani na marafiki wa kampeni itatembelea hospitali ya wagonjwa
wa saratani katika hospitali ya Ocean Road Cancer Institute tarehe 24 Novemba
2012 saa 4 asubuhi. Ili kufanikisha zoezi hilo imeomba watu binafsi na
makampuni mbali mbali na jamii kwa ujumla kuchangia misaada ya sabuni za
kufulia, za kuogea, mafuta ya kujipaka (petroleum jelly), miswaki, dawa za
miswaki, ndala, maji ya kunywa, juice mbalimbali na mtunda.
Tanzania 50 Plus Campaign inamshukuru
sana Mwalimu Florence Mboya kwa ukarimu wake na moyo wa upendo na huruma kwa
wale wenye mahtaji. Bado tunaendelea kupokea misaada.
Ukiwa na msaada wako wasiliana nasi:
Simu 0754
402033
au barua pepe: chrptz@yahoo.com,
ekandusi@yahoocom
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...