Umoja wa watanzania Ujerumani,unafuraha kutoa wito kwa wasanii
wa Tanzania wanaoishi nchini Ujerumani,wenye vipaji vya kupiga na
kuchenza ngoma za kiasili,sanaa za maonyesho kama sarakasi,
na waimbaji wa kwaya ,kujitokeza hili kuunda kikundi cha ngoma za
kiasili.
Wasanii tunawaomba muwasiliane na Mwenyekiti wa UTU
Wasanii wa Tanzania mnaoishi Ujerumani mnaombwa kutokalia
vipaji vyenu majumbani,tafadhalini tumieni nafasi hii kujitangaza
Kuutangaza utamaduni wa nchi yetu.mfano mnauona kwa wanamuziki
wa dansi wanajitangaza. Wasanii tumieni nafasi ,jitokezeni kwa wingi kuunda kundi.
Umoja ni Nguvu
Mfundo Peter Mfundo
Mwenyekiti(UTU)
email. kamati.utu@gmail.com
simu 01734292997
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...